Jifunze  kuandika barua ya maombi ya kazi

Jifunze kuandika barua ya maombi ya kazi

Umewekeza katika elimu yako, una kila sifa ya kupata kazi fulani lakini hupati kazi hiyo, inawezekana kabisa moja ya sababu inayokukwamisha ni kutokujua kuandika barua ya maombi ya kazi.

Basi leo katika karia tutakujuza jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi na itakusaidia wewe mwanafunzi pindi utakapomaliza na kuhitaji kuomba kazi ikupitishe moja kwa moja.

Barua ya maombi ya kazi huandikwa kwa malengo ya kuomba kazi tu hivyo kujifunza namna sahihi ya uandishi wa barua ya maombi ya kazi si kwamba itakusaidia katika kujibu maswali pekee, bali ujuzi huu utakufanya upate kazi halisi wakati utakapo hitaji kufanya hivyo.

Mimi binafsi nilishawahi kuitwa kwenda kufanya kazi mahali fulani na hiyo ni kwa sababu tu niliandika vizuri barua yangu ya maombi ya kazi.

Sasa nitakuelekeza yale unayotakiwa kuyafanya unapoandika barua ya maombi ya kazi, naomba ujifunze taratibu ili baadae uweze kuandika barua unayotaka na uweze kupata kazi.

Muundo wa barua ya maombi ya kazi

  1. Anuani ya mwandishi, yaani anuani yako wewe unayeandika barua hiyo.
  2. Tarehe
  • Anuani ya anayeandikiwa
  1. Salamu
  2. Kichwa cha Habari
  3. Kiini cha barua, hii ndio roho ya barua yako, ukikosea mahali hapa kama unajibu mtihani utapoteza alama. Na kama unaomba kazi halisi, utaikosa, na hichi kiini kina aya nne.

Katika aya ya kwanza, eleza kazi unayoomba na mahali ulipoona tangazo la kazi hiyo, katika sehemu hii unaweza kutaja umri wako.

Katika aya ya pili, eleza ujuzi wako kwa ufuli, Usieleze sana barua hii haipaswi kuwa ndefu kupindukia.

Kwenye aya ya tatu,eleza kwa nini upewe wewe kazi na si mtu mwingine, sasa hapa epuka kabisa kueleza shida zako binafsi ili upewe kazi.

Aya ya nne eleza kama uko tayari kwa usahili siku gani.

Mwisho wa barua yako lazima kuwe na neno la kufungia amblo ni wako mtiifu, wako katika ujenzi wa taifa

Sahihi yako na baadaae jina lako.

Pia barua ya maombi ya kazi huambatana na CV, hivyo utakapomaliza kujifunza jinsi hii ya kuandika barua hiyo jifunze pia namna ya kuandaa CV.

 

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post