Marekani kushuhudia kupatwa kwa jua

Marekani kushuhudia kupatwa kwa jua

Kwa mujibu wa #NASA ambao wanahusika na masuala ya utafiti wa anga kutoka nchini Marekani kupitia tovuti yao wameeleza kuwa Aprili 8, 2024, Marekani itashuhudia kupatwa kwa jua baada ya kupita muda mrefu bila tukio hilo kutokea.

Kupatwa kwa jua kutaonekana katika sehemu tofauti tofauti ikitokea Kaskazini mwa Mexico, Marekani na Canada ambapo tukio hilo linadaiwa kuchukua muda wa dakika 4 na sekunde 28.2.

Mara ya mwisho tukio la kupatwa kwa jua nchini Marekani lilitokea Agosti 21, 2017 likichukua muda wa dakika 2 na sekunde 40, kwa mujibu wa #NASA imeeleza kuwa mwaka huu tukio hilo litakuwa la kupendeza zaidi kutokana na kuchukua muda mrefu kuliko hapo awali.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post