Mambo ya kuzingatia kutunza uso wenye mafuta

Mambo ya kuzingatia kutunza uso wenye mafuta

Leo katika segment ya Fashion nimekusogezea dondoo zitakazo kusaidia wewe msichana au mvula ambaye unatatizo sugu la uso wako kuwa na mafuta mengi, hata usijali wewe endelea kunifatilia kwa makini tu.

Kwanza kabisa wengi wetu tunachukia kuwa na mafuta usoni yanayoenda kusababisha chunusi zisizo koma yaani chunusi sugu na kuharibika kwa ngozi.

Kimsingi hali hiyo huwa inakera, lakini chakushangaza pia ina uzuri wake ukiwa na uso wenye mafuta hahahahahaaa! najua hapa mtashangaa sana ila endelea kufatilia utajua tu namaanisha nini vipenzi vyangu mnaopenda Urembo na Fashion.

Usichokijua ni hiki uso wenye mafuta haushiki mikunjo haraka kama uso mkavu. Hii ndiyo faida moja wapo kubwa sana ya uso wa mafuta.


Sasa tuangalie njia za kutunza uso wenye mafuta

* Uso wenye mafuta lazima uweunaoshwa mara kwa mara na ‘facewash’ siyo sabuni za kawaida yaani kuna sabuni maalumu zinazopunguza mafuta usoni na huwa zinapatikana madukani kwa wingi au supermarket.

* Uso wenye mafuta unaoshwa mara 2 au 3 kwa siku hapa najua watu huwa wanaona uvivu kufanya hivyo au u-busy wa kazi lakini angalau ukifanya hivyo itasaidia ngozi ya uso wako kuwa namuonekano mzuri.



* Uso wa mafuta hautaki maji ya moto kabisa yaani mtu asikudangaje uso wa mafuta unaoshwa kwa kutumia maji ya moto maana ni sumu kwa uso wa mafuta kwa sababu yanazidisha joto na kuleta chunusi nyingi usoni.

* Uso wenye mafuta na wenye chunusi nyingi sana hautakiwi kufanyiwa scrub kwa sababu ukifanya scrub chunusi hupasuka na kutoa maji maji yanayosambaa na kuzalisha chunusi nyingi sana na pia kusababisha mafuta kutoka kwa wingi usoni.

* Uso wenye mafuta husababisha vipodozi kutodumu kwa muda unaotakiwa, unashauriwa kabla ya kupaka vipodozi usoni sugua uso na shingo kwa barafu baada ya hapo unapaka vipodozi.

* Njia rahisi ya kupunguza mafuta usoni pendelea kusugulia ndimu usoni. ndimu ina acid na hukata mafuta unashauriwa kukata ndimu kipande na kisha sugua usoni na ukae nayo mpaka ikauke kisha nawa na maji ya bomba au ukipenda maji ya baridi yaliyotoka kwenye ‘fridge’.


Pia unaweza kukamua ndimu za kutosha na kuchanganya na maji na kugandisha ikawa barafu kisha unasugulia usoni. Huleta unadhifu na kupunguza mafuta usoni na huondoa madoa pia.

* Uso wenye mafuta hautaki joto. Joto namaanisha lotion au mafuta ya aina yeyote yale ukipaka lotion au mafuta usoni ambapo tayari uso una mafuta huleta chunusi kwa wingi sana. Chunusi hizo hua ndogo ndogo au kubwa zenye usaha na huacha alama na mabaka usoni.

* Kama una safari ndefu basi tangulia siku moja kabla au shinda siku nzima na maji ya ndimu usoni na kabla ya kuanza kupaka vipodozi sugua barafu ya kawaida au ya maji ya ndimu na nawa kwa maji ya bomba au ya baridi kutoka katika fridge kisha paka vipodozi.

Kingine ambacho kitakusaidia katika uso wenye mafuta ni kuepuka kutumia vipodozi ambavyo vinamafuta hapa na zungumza na wale wanaokubali kupata ushauri kiholela kutoka kwa watu ambao hawafahamu mambo ya urembo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post