Malume awavaa wabongo, ishu za Eba Engonga

Malume awavaa wabongo, ishu za Eba Engonga

Msanii wa hip-hop nchini Moni Centrozone ‘Malume’ amewavaa Wabongo kwa kutosapoti muziki wa nyumbani na badala yake kilipa kipaumbele suala la kiongozi wa Guinnea Eba Engonga, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kingono zikihusisha video zaidi ya 300.

Kupitia mtandao wa Instagram Malume amechapisha picha iliyosindikizwa na maneno yakionesha kuwashangaa Wabongo kwa kushindwa kusapoti muziki nchini

"Mabraza wametoa album huko mnajifanya hamuoni mambo ya Eba engonga wa Guinnea mshashoboka ila wabongo mnadhambi sana, haya aliyekula kala aliyenawa kala mimi nishaondoka sijui mlotoa ngoma wiki hii,"kaandika Moni

Kwa wapenzi wa burudani mabraza hao wanaozungumziwa na Moni watakuwa wameelewa kwani Fid Q na Lord Eyes wanatarajia kuachia album ya pamoja itakayo fahamika kama ‘NENO’ yenye jumla ya ngoma 15 huku ngoma 7 tayari mashabiki walionjeshwa tangu November 2 2024 kwenye usiku wa Neno Experience ulioandaliwa kuwapa vionjo mashabiki, wadau wa muziki, viongozi wa serikali, mabalozi mbalimbali, wasanii na waandishi wa habari

Hata hivyo Malume ametumia sehemu hiyo kuonesha namna ambavyo wasanii watakaotoa nyimbo wiki hii pengine hazitopokelewa kwa ukubwa kutokana na tukio hilo ambalo linaendelea kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha hii sio mara ya kwanza kwa Malume kulia na wadau wa muziki nchini kutotoa ushirikiano kwenye muziki hususani wa Hip-hop, kwani katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya na Clouds Media alieleza namna ambavyo watu wengi Bongo wanavyopenda udaku.

Kwa sasa Malume anatamba na wimbo wake wa ‘pisi‘ ukiwa na version 2 Original akiwa mwenyewe na REMIX akimshirikisha Marioo, ikiwa na miondoko ya trap huku ukifanya vizuri Africa mashariki mpaka kufikia namba 4 kwenye audiomack nchini Burundi, pia kuwepo kati ya nyimbo 100 za Hip-hop zinazosikilizwa zaidi duniani kwenye mtandao wa audiomack






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post