Huyu ndiye ataiwakilisha TZ kwenye Miss Universe

Huyu ndiye ataiwakilisha TZ kwenye Miss Universe

Mwanamitindo Judith Peter anatarajia kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Universe 2024 yanayotarajia kufanyika nchini Mexico.

Mshindi huyo wa Miss Universe Tanzania 2024 tayari amewasili Mexico akiungana na washiriki wengine 19 kutoka katika mataifa mbalimbali kuliwinda taji la Miss Universe 2024.

Mbali na kushinda taji la Miss Universe Tanzania pia mlimbwende huyo amewahi kuondoka na taji la Miss United Nation mwaka 2022 huku akiingia tena kibaruani Novemba 17 mwaka huu katika fainali za shindano la Miss Universe.

Utakumbuka kuwa mwaka 2023 taji hilo lilichukuliwa na Sheynnis Alondr Palacios kutoka Nicaragua huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Annonia Porsild kutoka Thailand.

Judith ataungana na washindani wengine kutoka mataifa mbalimbali akiwemo mwanadada Chidimma Adetshina akiwakilisha Nigeria ambaye alizua gumzo kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na kutojulikana uraia wake halisi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags