Magonjwa yaendelea kumtesa Selena Gomez

Magonjwa yaendelea kumtesa Selena Gomez

Baada ya baadhi ya mashabiki kuhoji kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na kupungua mwili kwa mwanamuziki na mwigizaji kutoka Marekani Selena Gomez , hatimaye msanii huyo ameeleza kuwa anakabiliwa na tatizo la kiafya katika utumbo mdogo.

Mwonekano wake usio wa kawaida wengi waliuona katika uzinduzi wa filamu ya Netflix ‘Emilia Perez’ mjini Los Angeles, ambayo anacheza nafasi ya Muhusika Mkuu.
na kueleza kuwa anashida kwenye utumbo mdogo.

“Majadiliano haya yananifanya niwe mgonjwa, Nina (SIBO) kwenye utumbo wangu mdogo na ndio maana huwa linajaa, sijali kwa kuonekana kwangu mwembamba kama kijiti kwa sababu najijua sina mwili huo, nataka watu wajue kuwa, sio mwathirika mimi ni binadamu tuu kama wengine”, aliandika Gomez katika upande wa komenti inayosambaa mitandaoni

SIBO, ni ugonjwa unaosababishwa na ongezeko la bakteria ambao si wa kawaida katika eneo hilo la mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, kulingana na Mayo Clinic.

Hii sio mara ya kwanza kwa Gomez kuweka wazi kuhusiana na matatizo yake ya kiafya pia amewahi kuweka wazi kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa lupus.

Ikumbukwe kuwa Gomez alipandikizwa figo mwaka 2017 hata hivyo hivi karibuni alitangaza kuna na changamoto ya uzazi inayopelekea kushindwa kupata ujauzito kwa njia ya kawaida






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags