Baada ya kuwepo na ushindani katika muziki wa bongo fleva kumekuwa na maoni ya watu wengi kuwa ushindani huo uhamie katika #HipHop na mashabiki watoe ushirikiano kama wanavyoshabikia Bongo Fleva.
Kupitia tweet ya mtangazaji wa radio moja maarufu nchini, #Jabirsalehtherealest ameandika kuhusu wasanii wa hiphop kupewa ushirikiano pale wanapo raruana kwenye diss track, huku akitolea mfano wa mwanamuziki wa #HipHop #Rapcha_tz, kuwa ana kazi kubwa lakini kwa sababu sio diss track basi kuna ushirikiano anakosa.
#Jabirsalehtherealest kwenye ukurasa wake wa Twitter ameandika,
“Game ya #HipHop imechangamka, tunataka diss kama hizi, kauli hizi husikitisha sana, ku-suport rapa na wanahiphop ni mpaka wararuane na kuna wakati wanatoa ngoma kali, Rapcha ameachia mzigo mkali sana una mawe makali karibu yote, ila kwakuwa sio diss kama ile kwa D kimya”.
Leave a Reply