Kabati alilokuwa akihifadhia nguo marehemu Kobe Bryant, lililokuwa kwenye Uwanja wa Michezo wa Staples Center, uliopo Los Angeles, Marekani linapigwa mnada.
Kabati hilo ambalo Kobe alianza kulitumia kuanzia mwaka 2004 hadi 2016, linapigwa mnada katika jumba la Sotheby’s, ambalo hujihusisha na mauzo ya kazi za sanaa, vitu vya kumbukumbu, na mali nyingine za thamani.
Aidha kabati hilo ambalo limebeba kumbukumbu ya mchezaji huyo limewavutia wengi na linatarajia kuuzwa $1.5 milioni, Sh 3.9 bilioni. Sehemu ya mapato ya mnada itatumika kuchangia Msingi wa Vijana wa Los Angeles Lakers, kama kuendeleza urithi wa ufadhili wa Bryant.
Utakumbuka kuwa Kobe Bryant alikuwa mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu kutoka Marekani ambaye aliichezea timu ya Los Angeles Lakers katika NBA (Chama cha Taifa cha Mpira wa Kikapu). Alizaliwa mwaka 1978 na alifariki dunia kwa ajali ya helikopta Januari 26, 2020.
Bryant alikuwa mmoja wa wachezaji bora katika historia ya mchezo wa mpira wa kikapu, akiweza kushinda mataji mengi ya NBA. Mbali na mafanikio yake kwenye uwanja, pia alikuwa maarufu kwa juhudi zake za kijamii
Leave a Reply