Verse za pili kwenye ngoma za Alikiba ni asali kwa mashabiki

Verse za pili kwenye ngoma za Alikiba ni asali kwa mashabiki

Na Masoud Kofii

Licha ya kuwa ngoma za mwanamuziki Alikiba zimekuwa zikifanya vizuri na kupokelewa kwa mapenzi makubwa, lakini ngoma hizo zinaonekana kuwakuna zaidi mashabiki katika verse zake za pili.

'Utu'(2022)
Utu ya Alikiba kutoka kwenye album ya "Only One King" iliyotoka 2021 ni miongoni mwa ngoma kubwa za Bongo Fleva iliyopokelewa vizuri na mashabiki. Kwenye ngoma hiyo verse ya pili inaonekana kuwateka mashabiki wengi

"Siku zote maumivu maumivu yapo kutufunza tukipata furaha jinsi gani ya kuitunza, huko nyuma hukumu hukumu zilisha nifunza kwa mateso ya kung'ang'ania kupendwa usipopendwa
nilifosi kujificha kule kumbe chaka langu ni hapa sasa napewa amani mapenzi yasiyo na mipaka"

Mbio
Mbio iliachiwa 26 April 2019, wimbo unaoelezea hali ya mapenzi kwenda ndivyo sivyo mpaka kufikia hatua ya mwanaume/mwanamke kutaka kujitoa kwenye mahusiono, Na hapo ndio linapatikana jina la wimbo 'Mbio'.

"Are we still dating?, maana hueleweki, ama ndo nimechokwa, ama umetekwa,
nawaza na kufikiri, majibu sipati, na moyo unachosha akili, kwa mapenzi ya kufosi,
kupenda pasipo thamani,kwangu taabani si sawa ni bora unipe moyo wangu niufiche."

Mwana
Moja kati ya nyimbo bora sio tu kwa Alikiba hata kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa ujumla, ni Mwana iliyotoka Dec 19, 2014. Verse ya pili ya wimbo huu inaimbika

"Ukaanza kulewa madawa kuvuta kwa sana, ndani nya Dar Es Salaam, mambo matamu, hayakukuisha hamu, We bado mtoto kwa mama hujayajua mengi, wendetezi na omo marijio ngamani,
amesema sana mama dunia tambala bovu, kuna asali na shubiri ujana giza na nuru,"

Pamoja na yote hayo Alikiba anaendelea kuwa miongoni mwa wasanii wanaofanya vizui kutokea Tanzania tangu alipoanza muziki 2006 akiwa na album mbili na EP moja mpaka sasa ambazo ni Cinderalla, Only One King, na EP ni STATER






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post