Miaka 45 ya staa wa Tittanic katika ulimwengu wa filamu

Miaka 45 ya staa wa Tittanic katika ulimwengu wa filamu

Leonardo DiCaprio ndilo jina halisi la nyota wa filamu Tittanic, ambaye wengi wanamfahamu kama Jack Dawson kutokana na uhusika wake kwenye filamu hiyo. Mkali huyo ambaye jana Novemba 11 alitimiaza umri wa miaka 50 tangu kuzaliwa kwake, hadi sasa amefikisha miaka 45 ya kutumikia kiwanda cha filamu hivyo anakuwa kati ya wasanii wachache duniani waliotumikia kiwanda hicho kwa muda mrefu.

Leonardo ambaye kwa sasa anazaidi ya miaka 45 katika tasnia ya uigizaji kutokana na kuanza kuigiza akiwa na umri mdogo. Alianza kwa kuonekana kwenye matangazo ya biashara (commercials) na programu za televisheni akiwa mtoto wa miaka mitano. Baada ya hapo, alijitokeza katika vipindi maarufu vya televisheni kama 'Parenthood' (1990), kabla ya kupata nafasi kubwa zaidi kwenye filamu.

Akiwa na miaka 14 alishiriki kwa mara ya kwanza katika filamu ya 'Critters 3' iliyotoka mwaka (1991) na 'Critters 4' (1992), lakini alijulikana zaidi baada ya kuonekana katika filamu ya 'This Boy’s Life' (1993), ambapo alicheza pamoja na Robert De Niro, na 'What’s Eating Gilbert Grape' (1993), ambayo alicheza na Johnny Depp.

Hata hivyo kuonekana kwake kwenye filamu hizo kulimpa shavu na kumfanya ageuke kivutio katika filamu maarufu 'Titanic' (1997), ambapo alicheza kama Jack Dawson, na alijipatia umaarufu wa kimataifa. Filamu hiyo ilivunja rekodi za kimataifa na kumfanya kuwa mmoja wa waigizaji maarufu duniani.

Mbali na filamu hiyo aliendelea kuonekana kwenye filamu nyingine maarufu kama 'Inception' (2010), 'The Wolf of Wall Street' (2013), 'The Revenant' (2015), na 'Once Upon a Time in Hollywood' (2019).

Pamoja na umahiri wake katika uigizaji, DiCaprio pia ni mtafiti na mhamasishaji mkubwa katika masuala ya uhifadhi wa mazingira. Ameanzisha taasisi yake ya Leonardo DiCaprio Foundation, inayolenga kulinda mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa ufanisi wake katika sanaa ya uigizaji, DiCaprio ameshinda tuzo kadhaa, ikiwa ni pamoja na Tuzo la Academy (Oscar) kama Best Actor kwa filamu 'The Revenant' mwaka 2016. Leonardo alizaliwa Novemba 11, 1974, mjini Los Angeles, California.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post