Jinsi ya kutengeneza ubuyu kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kutengeneza ubuyu kwa ajili ya biashara

Nawasalimu kwa jina la ubuyuu, semeni basi biashara ziendeleee, na hapa hatuzungumzii ubuyu ule mnaoujua nyie wa umbea hapa nazungumzia kufanya biashara, kutafta hela kwa kuchakarika.

Sasa leo katika biashara bwana nawasogezea biashara ambayo ukiitizama kwa mtaani mtaani watu wengi waidharau lakini nawaambia katika haya maisha hakuna biashara ambayo haina faida, usijali watu wanazungumzia nini kuhusu hicho unacho kifanya.

Biashara ya ubuyu ni biashara ambayo ni yamtaji mdogo na kwa kuanza pia ni yenye mtaji mdogo pia lakini, kwa kuanza sio mbaya, mwanzo kabisa kipindi naanza kufanya biashara hii ya ubuyu sikuwa nautengeneza mwenyewe nilikuwa naagiza kutoka Zanzibar kwa Babu Issa, lakini toka nifundishwe kutengeneza nimekuwa mwalimu.

Leo hapa tutaelekezana kutengeneza ubuyu kwa ajili ya biashara, angalizo kabla haujaenda kuanza ni inabidi uanze kujifunza kutengeneza hata mara tatu au mara mbili na uwape watu wako wa karibu wao ndo watakupa majibu kama uko sawa au laa, na ukiuona unaweza anza kutengeneza kwa ajili ya kuuza.

MAHITAJI 
Sukari vkombe 2
Maji vikombe 2
Nusu kikombe cha unga wa ubuyu
Vikombe 4 vya ubuyu msafi usiokuwa na mchanga
1/4 Pilipili ya unga (sio lazima kuweka ubuyu)
1/4 tsp Chumvi
1/4 tsp iriki ya unga
 Rangi nyekundu au wewe utakayopendelea 

HATUA YA KWANZA

Tayarisha sufuria na uwekemaji jikoni na weka chumvi, sukari, pilipili ya unga, Rangi na iriki ya unga kwa moto wa juu kisha changanya vizuri. 

Wakati vinaendelea kupikika utakuta rojo linatoa mapovu endelea tu kukoroga kisha acha rojo liendeleee kupilika vizuri, kisha chukua mwiko wako kisha angalia rojo linanata huwa linatakiwa linate kama halinati ujue bado jojo lako halijaiva utaliacha mpaka uonee linanata. Hapa ni kama unavyotengeneza shira nadhani wote tunaelewa kuhusu shira ya kuweka katika visheti basi na katika ubuyu inabidi iwe hivyo hivyo.

Baada ya hapo chukua ubuyu wa kokwa mimina kisha koroga vizuri kama dk 2 hivi kisha mimina tena unga wa ubuyu na uendelee kukoroga Endelea kukoroga mpaka sukari inaanza kuganda ukiona hivyo basi weka pembeni umimine upoe hapo tayari ubuyu wako upo tayari  kwa kufunga kwa kuliwa na biashara.

Angalizo: hapa watu wengi wanaweza kuona ni kitu chepesi haswa kwa maelezo, ndio maana nikasema inabidi ujaribu kama mara 3 au nne ujirizishe kama kweli umeshakuwa fundi mzuri wa kutengeneza ndo uanze kuwauzia watu.

Kama tunavyojua biashara ni biashara kama unaona ni ngumu kufanya hivyo basi agiza tuu kutoka Zanzibar nawewe ufanye biashara yaani huu mwaka sio wa kukaa kizembe. Nasemajeee nasemajeee tukutane tena next week watu wangu wa nguvu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post