Mambo vipi mdau karibu kwenye ukurasa wa Nipe dili bwana kama kawaida hua hatuachi kitu kabisa hapa ni kufundisha na kuelekezana jinsi ya kupika vyakula mbalimbali.
Leo kwenye ukurasa huu tutaelekezana namna ya kupika pilau la nyama sio ilimradi pilau bwana embu andaa chakula kizuri ambacho kitakupa fursa ya kupata walaji kila kukicha karibu.
Bila kupoteza muda twende kwenye orodha ya viungo sasa.
- Mchele kilo1 ¼
- Nyama kilo ½
- Mafuta yakupikia lita ¼
- Njegere kilo ½
- Giligilani pakti ndogo 1
- Mdalasini ya unga packti ndogo 2
- Jira packti ndogo 2
- Chumvi packti ndogo 1
- Vitunguu-maji kubwa 3
- Vitunguu-saumu kubwa 1
Hatua inayofuata sasa ni mataarisho ya viungo vyako sasa fuatilia kwa makini kabisa ukisha andaa vitu vyote hivi basi jua tayari umefanikiwa.
- Anza kumenya vitunguu saumu
- Katakata vitunguu maji
- Chambua girigilan
- Kata kata nyama
- Chukua vitunguu swaumu, girigilan, jira viweke kwenye
- kiuri na utwange vizuri hadi vilainike
Hatua na maelekezo ya kupika
- Chukua sufuria yako bandika jikoni weka mafuta
- Weka vitunguu maji jikoni
- Kaanga hadi viwe na ranging ya kahawia
- Weka nyama anza kuikaanga
- Endelea kugeuza nyama yako ikaange vizuri hadi iive
- Chukua mchanganyiko wa vitunguu swaumu, girigilan, jira ulio twanga viweke na endelea kukaanga
- Chukua mdalasin weka koroga vizuri
- Weka chumvi geuza
- Weka njegere zako geuza vizuri ichanganyike
- Weka maji acha ichemke kwa dakika tano
- Weka mchele geuza vizuri taraaraatibu
- Funika na uweka moto mdogo wakuivisha chakula taratibu kwa dakika kumi
- Funua chakula chako geuza hapo kitakua pilau iliyo tayari kwa kula
Nikukumbushe tu kuwa upishi wa pilau uko wa aina nyingi hivyo basi ubunifu wako ndiyo utakaokuletea matokea mazuri.
Leave a Reply