Hellow! kama tulivyo kubaliana ni mwendo wa kufanya biashara tu mpaka uchumi ukae sawa ama mnasemaje wachakarikaji wenzangu? yani ni mwendo wa kushushiana vitu konki kama mnavyojua kwenye sekta hii hatunaga mba mba mba.
Sasa niwape story bwana hakuna mkate ninao upenda katika maisha yangu kama huu wallah! nikajua peke yangu bwana nikafanya uchunguzi kwa baadhi ya marafiki zangu nao pia ni walevi wa kitafunwa hichi.
Kama kawaida yetu kabla hujatengeneza mkate huu kwa ajili ya biashara unatakiwa utengeneze mara mbili au tatu ili kujihakikishia kama kweli umekuwa fundi na vitu vyako unavyotaka kuviuza kama vinaubora.
MAHITAJI
- Mchele kikombe 1
- Nazi ya unga kikombe 1
iii. Sukari kikombe kimoja 1
- Kikombe 1 cha maji au maziwa ya vuguvugu
- Kijiko 1 cha chai cha hamira
- Iliki kiasi upendavyo
vii. Ute wa yai moja
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
- Osha na loweka mchele siku moja ndani ya maji ya baridi.
- Saga ndani ya blender, mchele, tui, maji au maziwa, iliki, na hamira mpaka mchanganyiko uwe laini kabisa.
iii. Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko wako uumuke.
- Mchanganyiko ukiumuka,washa ovener kabisa ili ipate moto wa 350°. Mimina sukari pamoja na ule ute wa yai ndani ya mchanganyiko na uchanganye vizuri.
- Ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
- Chukua sufuria umimine mafuta kidogo. Washa jiko na uweke sufuria ipate moto kiasi.
vii. Mimina ule mchanganyiko ndani ya sufuria uuwache kama dakika 5 hivi kiasi mkate uanze kushikana.
viii. Funika sufuria na bake ndani ya ovener kama dakika 35-40 hivi, au mpaka mkate uive na uwe rangi ya udhurungi juu yake.
Cha msingi cha kuzingatia ni kuuepua na uache upoe kabisa kabla ya kukata na mchele mzuri wa kuutumia ni VIP au Pisholi. Na kwa wale wenzangu wa majiko ya mkaa unaweza tuu kuupalilia kama wali lakini kwa moto mdogo sio moto mkubwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply