Fanya haya kuvutia wateja kwenye biashara yako

Fanya haya kuvutia wateja kwenye biashara yako

Wajasiliamali oyee! Leo niko na ka-vibe fulani hivii ka kuwapa mada ambazo zitakufanya upate maokoto kwa wepesi kwako wewe mfanyabiashara mwenzangu, unataka kujua unapataje maokoto basi ungana nami mwanzo mpaka mwisho katika segment yako pendwa ya Biashara.

Nimekutana na malalamiko kadhaa kwa baadhi ya wafanyabiashara wakilalamika biashara zao kutofanya vizuri siku hizi, na hata wateja walionao hawarudi tena kununua biadhaa zao, unataka kujua nini kinasababisha hivyo endelea kusoma hapo chini.

Kama tunavyojua biashara ina-risk sana usikae kizembe kupata maokoto kupitia kufanya baishara, siyo kama kuchemsha maji ya kuoga kuwa kila mtu anajua, bali kuna time inahitajika uwe muongo, uwe mkweli, ujitoe na ukubaliane na changamoto zote.


Toa ofa mara kwa mara
Tunajua kabisa inaweza kukusababishia biashara yako kuyumba lakini jambo la msingi ambalo linaweza kukufanya upate maokoto kwa wepesi na kuwavutia wateja ni kutoa ofa kwa wateja.

Waswahili wanasema wateja wafalme, basi huu ndio ufalme wenyewe wateja wanahitaji mambo kama haya unaweza kupunguza bei, au hata kufanya nyongeza kwa bidhaa unazoziuza.
Njia hiyo itakusaidia kupata wateja wengi na waweze kurudi mara kwa mara licha ya kuwa hauingizi kubwa ila ni nzuri kuitumia kwa kuanzia biashara yako kwani itakuletea matokea chanya na kupanua wigo kwa upande wako.

Wafanye marafiki zako kuwa wateja wako.
Hii inaweza kuwa ngumu kutokana na kila mtu anamarafiki wake, na katika hao marafiki ulionao huwezi kujua yupi na yupi anayeweza kukusaidia kutangaza bidhaa yako kwa marafiki zake, lakini unaweza kuwachangua hata watano kwa kuanzia.

Itakusaidia sana kuendelea kupata wateja wale wale ambao ikifika kipindi cha muda fulani ndiyo watakuwa ambassador wako wazuri bila hata ya kuwalipa. Na hii yote inakuja kutokana na kuwa na lugha nzuri kwa wateja.

Epuka majibu ya mkato kwa wateja wako, weka uso wa bashasha na tabasamu kwa mteja kwani mara nyingi wateja huvutiwa na vitu vidogo sana kwenye biashara yoyote ile.

Hakikisha unakuwa mvumilivu kijana mwenzangu hapa nisome kwa umakini kabisa ili uwe mfanyabiashara mzuri hii ngao ya uvumilivu usiiache ikumbatie kadri uwezavyo kwani ndiyo nguzo muhimu ya kufanikiwa kwenye shughuli zako.

Wengi wanashindwa kuendeleza biashara zao kwa sababu ya kukosa uvumilivu hakuna mafanikio ya harakaharaka ‘There is no sweet without sweat’ simamia msemo huo hakuna kitu chepesi.


Wafahamu wateja wako
Fahamu mambo kadhaa kuhusu mteja wako kama, anapenda nini, nini ukimjibu anakwazika, anahitaji vitu gani, in short lugha nzuri ndiyo kila kitu kwani ndiyo kipimo chako kwa wateja.

Mteja anapokuja kukulalamikia uwe mvumilivu chukua muda wa kumsikiliza mteja, kuwa na subira na usikilize kila wanachokisema, mwisho muombe msamaha na kumuahidi kuwa haitojirudia tena. Unatakiwa ukwe msikilizaji kuliko muongeaji.

Tunajua kila mtu ana hasira lakini kwenye biashara inabidi kuzuia hasira zako kwa wateja, biashara inahitaji uaminifu, nidhamu na kumsikiliza mtaje kwa kina zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post