Ijue balehe ya ndoa

Ijue balehe ya ndoa

Najua kuwa vijana wenzangu mliopo vyuoni mnatamani siku moja kuoa au kuolewa lakini mnafahamu balehe ya ndoa?

 

Leo katika dondoo ya saikolojia tutaongelea balehe ya ndoa ambayo kiutaalamu ni kipindi cha mpito ambacho wanandoa wengi lazima wapitie.

 

Kipindi hiki uwa ni cha miaka mitano ya mwanzo ambacho kwa wale wanandoa werevu wataweza kutengeneza ndoa wanayoitaka na kuweza kujua itaweje siku zote.

 

Ni kipindi ambacho kila mmoja anamsoma mwezake kwa undani zaidi na uonyesha misimamo na mitazamo yake ambayo inaweza kuwa ya tofauti.

 

Hata hivyo mitazamo hiyo ndio inasababisha kutofautiana na kushindwa kuelewana na hapo ndipo ndoa inaweza kutengenezwa kama mmoja wapo atakuwa na hekima na kujishusha.

 

Jambo hilo likifanyika ndoa hiyo inaweza kuduma na lisipofanyika haitaweza kudumu wala kufika popote pale.

 

Tunajua vijana wengi kwa sasa wanafunga sana ndoa licha ya kutambua vitu kama hivyo ndio maana leo katika dondoo hizi tueleze haya ambayo ni manufaa kwa wanadoa na watarajiwa.

 

Matarajio unapoingia kwenye ndoa

 

Kila moja anapoingia kwenye ndoa anakuwa na matarajio yake lakini anapoingia na kuona vitu tofauti na ambavyo ametegemea shida ndipo uanzia hapo.

 

Unakuta anakutana na mwanamke au mwanaume mwenye gubu kupita kiashi mpaka kuwepo nyumbani anaonashida ndipo pale anapotafuta mchepuko ili kuondoa msongo wa mawazo.

 

kipindi hiki watu wanakuwa na sonona kuliko kawaida kwa sababu ulitegemea mtakuwa marafiki na mmeo au mkeo unashangaa ni maadui hamuwezi hata kuakaa Pamoja.

 

Ndugu balehe ya ndoa ni kipindi ambacho unakuta kila mmoja bado hajaweza kuondoka katika familia ya kwao na kuanza kutengeneza familia yake.

 

Pia ni kipindi ambacho kila moja anasikiliza upande wa kwao, kwa hapo shida nyingi utokea upande wa mwanaume ambaye unamkuta  hawezi kuwawekea ndugu zake mipaka katika ndoa yake.

 

Ndoa nzuri inatengenezwa jamani, mke au mme wa ndoto yako ndio huyo huyo unaweza kumtengeneza akawa mke au mume bora katika ndoa yako.

 

Ukishindwa tafuta msaada wa wataalamu wa mambo ya saikolojia. Naamini ambao hawajaingia kwenye ndoa au wachanga kwenye ndoa wanapitia kitu

 

Naomba niishie hapo hili somo lina mambo mengi sana.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post