Ifahamu masaji inayofanywa kwa kupigwa makofi
Kawaida imezoeleka masaji hufanywa taratibu kwa lengo la kuondoa uchovu,lakini hilo ni tofauti kwa masaji ya kichwa ambayo inafanyika kwa muhusika kupigwa makofi kichwani.
Makofi hayo si adhabu bali ni masaji ambayo hupendelewa kufanywa na watu wa India katika mji wa Pushkar ambapo hujulikana kama ‘Cosmic head massage’ iliyoanzishwa miaka 2000 iliyopita.
Masaji hiyo inaelezwa kuwa ni mbinu ya tiba ya Ayurvedic inayohusisha kupiga makofi kichwani kwa mteja, makofi ambayo huwa tiba na si maumivu kama watu wanavyotafsiri. Utalipia dola 1 ikiwa ni zaidi ya Sh 2500 kwa ajili ya kupata matibabu.
Masaji hii inasemekana kulenga njia za nishati mwilini, kukusaidia kuwa na maisha marefu na kusaidia kupunguza maumivu ya misuli, kwa kawaida hufanywa huku mteja akiwa amevaa nguo kikamilifu na ameketi kwenye kiti.
Hata hivyo masaji haya yanatajwa kusaidia baadhi ya watu wanaosumbuliwa na kipandauso, majeraha ya shingo, hivyo huwa na manufaa katika kichwa kama kupunguza msongo na wasiwasi, kuboresha mzunguko wa damu na kuondoa sumu mwilini, kukuza ustawi wa mwili na akili na kuboresha hali ya ngozi ya kichwa na nywele.
Leave a Reply