Patoranking, Bien kwenye album ya Marioo

Patoranking, Bien kwenye album ya Marioo

Baada ya kusubiliwa kwa hamu orodha ya ngoma zilizopo kwenye albumu ya mwanamuziki Marioo, hatimaye orodha hiyo imeachiwa rasmi huku mwanamuziki wa Nigeria Patoranking akiwa ni miongoni wa wasanii walishiriki katika album hiyo.

‘The God Son’ ya Marioo inatarajiwa kutoka hivi karibuni ikiwa na nyimbo 17 huku wasanii mbalimbali akiwemo Alikiba, Harmonize, Kenny Sol, Aslay, Joshua Baraka wakiwa wamesikika



Marioo alitangaza ujio wa albumu hiyo mpya mapema mwaka huu huku akisisitiza kuwa na nyimbo zenye sound tofauti na iliyozoeleka Bongo.

Hii itakuwa album ya pili kwa msanii huyo kwani mwaka 2022 aliachia album aliyoipa jina la ‘The Kid You Know’ iliyokuwa na nyimbo 21.

Album hiyo imependezeshwa na ngoma kama Allhamdulillah, Why, Hakuna Matata, 2025, Wangu, Salio, Unanichekesha na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags