Sanaa ya upishi kukuza utamaduni, Waziri Pindi Chana agusia utalii

Sanaa ya upishi kukuza utamaduni, Waziri Pindi Chana agusia utalii

Kutokana na sanaa ya upishi kuwa miongoni mwa mambo yanayoweza kukuza na kuendeleza utamaduni, utalii, na uchumi. Kufuatia madhimisho ya msimu wa tisa wa wiki ya Vyakula vya Kiitaliano Duniani iliyoanza Novemba 16 hadi 23, 2024 Ubalozi wa Italy umeandaa matukio mbalimbali ikiwemo uonjaji wa vyakula vyenye asili ya kiitaliano.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 19, 2024 Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Pindi Chana amesema hivi sasa utalii unachangia takribani 17% ya pato la taifa lakini fedha za nje 25%, huku shilingi ya Tanzania ikianza kuimarika kutokana na wageni wengi kuingia nchini.



"Nichukue nafasi hii kuendelea kumshukuru muheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan, Rais ambaye ametoka yeye mwenyewe ofisini na kutengeneza filamu ya Tanzania The Royal Tour na sisi tunamaelekezo ya kuongeza watalii wasiopungua takribani milioni 5 ifikapo 2025 tunamaelekezo ya kuongeza mapato ya nchi kufikia dola zisizopungua dola 6 bilioni ifikapo 2025, tunaposema kuongeza watalii na fedha ni pamoja na huduma mbalimbali zinazoenda sambamba na kuhudumia watalii.

"Tupo hapa kushuhudia makubaliano 'Memorandum of Understanding' kati ya sisi na wenzetu wa Italy makubaliano ambayo yataongeza ujuzi, ufahamu wa vyakula vya aina mbalimbali, lugha lakini siyo tu Italy hata mataifa mengine,"amesema Waziri

Hata hivyo, katika kukuza na kubadilishana utamaduni, Ubalozi wa Italia umeingia makubaliano na Chuo Kikuu cha Utalii cha Taifa, makubaliano ambayo yataongeza ujuzi na ufahamu wa vyakula vya aina mbalimbali, lugha, na utamaduni wa Italia na mataifa mengine.

Balozi wa Italia nchini Tanzania, Giuseppe Sean, amesisitiza kuwa makubaliano hayo yatasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya ENAIP, taasisi kubwa ya Kiitaliano inayojulikana kwa uzoefu wake katika sekta ya utalii, na Chuo Kikuu cha Utalii cha Taifa.

"Tutaweza kuboresha mitaala ya mafunzo, kutoa mafunzo kwa wakufunzi na wanafunzi, na kujenga uwezo kwa pande zote.Tuna furaha pia kushirikiana na Tanzania katika kukuza sekta ya utalii, ambayo ni muhimu sana kwa nchi hizi mbili, na hasa kwa vijana. Sekta hii inatoa fursa za ajira kwa vijana na ina athari kubwa kwa maendeleo ya sekta zingine kama vile kilimo na uvuvi, kwani vyakula bora vinavyotengenezwa kutoka kwa mazao ya kilimo na uvuvi vya Tanzania vitatumika kuboresha huduma za utalii,"amesema Sean



Akielezea madhumuni ya wiki ya vyakula, Balozi Sean amesema, ni sherehe ambazo zilianzishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia miaka tisa iliyopita. Lengo kuu ni kukuza ujuzi wa vyakula vya Kiitaliano, ambayo ni sehemu muhimu ya urithi wa kitamaduni. Vyakula vya Kiitaliano ni muhimu si tu kwa ladha, bali pia kwa afya, kwa kuwa ni sehemu ya Mediterranean Diet, ambayo ni urithi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),"amesema Sean






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags