Hereni za Morgani ni maandalizi ya kifo chake

Hereni za Morgani ni maandalizi ya kifo chake

Kupanga ni kuchagua hivi ndivyo unaweza sema kwa mwigizaji maarufu wa Marekani, Morgan Freeman, ambaye amechagua hereni zake kuwa msaada siku akifariki dunia.

Katika kuchagua hilo sehemu yoyote ile anayoonekana Morgan huwa amevalia hereni zake masikioni, jambo ambalo limegeuka kuwa utambulisho wake.

Katika mahojiano aliyowahi kufanya na kipindi cha televisheni cha 'The Late Show with Stephen Colbert' mwaka 2014, Freeman alieleza kuwa hereni hizo ni za kipekee na anaamini kuwa zenye thamani ya kutosha kulipia jeneza ikiwa atafariki akiwa mahali ambapo itakuwa vigumu kupata msaada wa haraka.

Aliweka wazi hereni hizo ni muhimu kwake, si tu kama mapambo, bali pia kama kifaa cha kiusalama katika maisha yake ya kila siku.

"Navaa hereni hizi kwa sababu zina thamani ya kutosha kulipia jeneza langu endapo nitafariki mahali ambapo sina uwezo wa kumudu gharama za mazishi," alisema Freeman

Aliendelea kusema kuwa ingawa wengi wanavaa hereni kama sehemu ya mapambo, kwake yeye ni ishara ya kuelewa na kuthamini maisha kwa undani, na kwamba hereni zake zina umuhimu wa kipekee katika maisha yake.Hata hivyo hakuweka thamani halisi ya kifedha ya hereni hizo

Hata hivyo, Freeman aliyezaliwa June 1, 1937 ameendelea kuonekana kama mfano wa mtu ambaye anapenda kufikiria kwa kina kuhusu maisha ya sasa na yajayo. Kati ya filamu ambazo amecheza ni The Shawshank Redemption (1994), Se7en (1995), Bruce Almighty (2003),Kiss the Girls (1997)

The Bucket List (2007),Going In Style (2017),Lucy (2014),Now You See Me (2013), The Dark Knight (2008) na nyingine nyingi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags