
Jux: Nilipanga Kufanya Sherehe Rwanda Lakini Priscy Amechoka
Baada ya sherehe iliyosimamisha nchi ya Nigeria na Tanzania kwa wakati mmoja ya mwanamuziki Juma Jux na mke wake Priscilla Ojo, sasa wawili hao kufanya sherehe nyingine Bongo.
Taarifa ya kufanya sherehe hiyo imethibitishwa na Jux huku akieleza kuwa alipanga sherehe hizo ziendelee katika nchi mbalimbali lakini haiwezekani kutokana na uchovu.
“Mei 28,2025 tutakuwa na reception ya JP2025 na itakuwa ya mwisho kwa sababu mke wangu amechoka na heka heka za sherehe. Plan yangu ilikuwa ni kufanya sherehe Rwanda kwa sababu ndio sehemu tuliyokuta kwa mara ya kwanza.
Ila haiwezekani kwa sababu ya uchovu. Nilitamani kufanya sherehe sehemu mbalimbali kama, China, Kenya, USA na Uganda,”amesmea Jux
Uhusiano wa wawili hao unadaiwa kuanza mwishoni mwa mwaka 2023 lakini waliuweka wazi Agosti 2024 huku mambo yakishamiri zaidi baada ya Jux kwenda ukweni Nigeria ambapo alipokelewa kwa shangwe na mkwe wake ambaye ni mwigizaji mkongwe Nigeria Iyabo Ojo.
Hatimaye, Februari 7, 2025, wawili hao walithibitisha mapenzi yao kuwa ya kweli ambapo walifunga ndoa ya Kiislamu. Ikawa moja ya harusi kubwa zilizovuta hisia za mashabiki kutoka Tanzania, Nigeria, na kwingine.
Mbali na sherehe hiyo lakini pia walifanya shughuli nyingine iliyofanyika Nigeria ikiwa ni harusi ya Kitamaduni pamoja na kufunga ndoa ya kikristo huku wakisimamisha mitandao ya kijamii Afrika Mashariki.
Leave a Reply