Diamond anyoosha mikono juu kutochaguliwa Grammy

Diamond anyoosha mikono juu kutochaguliwa Grammy

Baada ya mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Diamond kutochaguliwa kuwania tuzo za Grammy, hatimaye msanii huyo amefunguka kwa mara ya kwanza akieleza kuwa atarudia tena huku akiamini ipo siku atashinda tuzo hizo.

Simba ameyasema hayo wakati akiwa kwenye hafla yake iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Novemba 20, 2024, Mlimani City jijini Dar es Salaam, kwa kusema wadau wake hawapaswi kuchukia kwa kukosa kuwania tuzo hizo kwani huwenda walifanya makosa katika uwasilishaji.

“Unajua jukumu langu mimi kama msanii kuhakikisha nafanya kazi bora na kuingiza kwenye mashindano na pale unatakiwa kukubali kwamba sio kila wakati utafanikiwa tunapokuwa hatujafanikiwa tusichukie tuongeze kasi, juhudi na kujifanyia tathmini ni sehemu gani tumeteleza.

“Mimi ni miongoni mwa watu ambao nikikaa na timu yangu ikitokea kitu chochote hatujakipata wakianza kulalamika mimi sipendi nawaambi aaah, pale tafsiri yake hatuko sawa either katika kazi yetu tuliyofanya, ama fitina ama connection pengine hatujamuomba Mungu sana. Kwa hiyo lazima ukubali kuwa kile mwenyezi Mungu amekipanga kisikukatishe tamaa ukaanza kuchukia watu, kutukana, kusema vibaya jitathmini mwenyewe weka dongo lingine mambo yatanyooka,” amesema Diamond

Hakuishia hapo aliongezea kwa kuwataka watu wasikate tamaa kwani huenda mwakani wakaondoka na tuzo 10 za Grammy.

“Kuna watu wengi kwa bahati mbaya pia hawakuchaguliwa na wamefanya vizuri sana kwa sisi tuamini kwamba tumefanya kazi bora tumepata mwanzo mzuri wa kuifungua dunia sasahivi ni kumwaga mawe mengi Mungu pengine katuandikia mwakani. Labda hatuingii tu kwenye kategori tutaondoka na 10 pale mimi naamini sana kwenye kila kitu kinawezekana, sasa inapotokea kitu umekikosa sio uanze kuchanganyikiwa na maneno ya watu huko mtandaoni hapana jenga tena mkakati wako”, amemalizia Diamond

Utakumbuka mapema Octoba,2024 Diamond aliwasilisha wimbo wa ‘Komasava’ uliotazamwa zaidi ya mara milioni 29 kwenye mtandao wa YouTube. Lakini mambo yamekuwa magumu upande wake kwa jina lake kutotajwa kuwania tuzo hizo katika vipengele alivyoorodhesha.

Diamond aliwasilisha jina lake kupitia wimbo wa 'Komasava' katika vipengele viwili, kwanza Video Bora (Komasava) na Mtumbuizaji Bora kutoka Afrika.

Hii siyo mara ya kwanza kwa msanii Diamond kuingiza nyimbo zake katika tuzo hizo, utakumbuka kuwa mwaka 2020 aliingiza wimbo wake wa ‘Jeje’ na Baba Lao katika Kinyang’anyiro hicho na kuishia hatua ya kwanza iitwayo ‘Consideration’.

Remix ya wimbo wa ‘Komasava’ mpaka kufikia sasa imetazamwa zaidi ya mara milioni 29 katika mtandao wa YouTube huku original yake ikiwa na watazamaji milioni 7.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags