Hekaheka za Khaligraph Jones na Watanzania

Hekaheka za Khaligraph Jones na Watanzania

Kama tunavyofahamu kauli ya Kaligraph iliwatoa wasanii wengi wa hip-hop kwenye mashimo waliyokuwa wamejificha, bidada Rosa Ree akaachia  mkwaju huku maneno kwenye mitandao ya kijamii yakiwa yanaendelea.

Katika jambo hili kila mtu amekuwa na mawazo yake sisi hatujakaa kinyonge tumekusogezea baadhi ya mawazo ya mashabiki wa muziki huo na tutaona wao wanazungumza nini kuhusiana na jambo hilo.

Kwanza kabisa kwa upandwa wangu naona jambo alilofanya mwanamuziki huyo wa Kenya sio jambo baya badala yake amewakumbusha wasanii wa hip-hop Bongo kujua nini wanafanya, hasa kulingana na msimu huu ambao muziki wa Amapiano umetawala dunia.

Moja kwa moja Mwananchi Scoop tulifuika kwa wadau mbalimbali wa muziki huo ili kupata maoni yako kuhusiana na kauli ya Khaligraph kupitia swali lililouliza, je alichafanya mwanamuziki huyo kimechangamsha muziki huo au hakina faida yoyote?.

Huyu hapa mdau wa Hip-hop Peter Minja anatueleza kuwa alichofanya mkali huyo kutoka Kenya kinamaana kubwa kwani kimekuja kuchangamsha muziki huo, mara nyingi waimbaji wa hip-hop huwa hawapati air time kama ilivyo kwa wasanii wa Bongo Fleva

Peter aliendelea kwa kusema kuwa mara nyingi wasanii wa hip-hop huzungumziwa kama tu wakifanya dis track huku akitaja baadhi ya mifano kama vile Rapcha na Dizasta Vina, Young Killer na Young Lunya.

Kwa kumalizia shabiki huyu alidai kuwa wasanii wa hip-hop ni wachache sana wanaojadiliwa katika muziki huo kwa hiyo kauli hiyo imewafanya baadhi ya wasanii waweze kurudi kama vile Fresh like a amesikika baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kwa hiyo kuachana na kauli ya kusema wasanii wa Bongo hawavai vizuri na kukisema Kiswahili basi kwa upande wa muziki kuwasema wasanii ni jambo zuri na limechangamsha game.

Haya habiki huyo kwa upande wake aliamua kuegemea kwenye mawazo chanya kuwa Khaligraph kaupiga mwingi na kachanamsha game, lakini hatukuishia hapo tukafunga safari hadi kwa shabiki mwingine huyu hapa.

Kwanza kabisa huyu  ni bidada anafahamika kama Casandra kwa upande wake akaegemea kumtete Khaligraph kwa alichofanya na kudai kuwa msanii huyo amefanya jambo jema kwani muziki huo umerudi nyuma wasanii wanakimbilia kwenye Amapiano ili wapate hela ya kula hawana tena mashairi mazuri na akaamua kumtole mfano Fid-Q kuwa kwa upande wake sasa hivi haachii ngoma tena kama ilivyokuwa mwanzo.

Casandra akamalizia kwa kudai kuwa kauli ya mwamba from Kenya ni jambo zuri kwani wasanii wataibuka ili kutaka kujidihilisha kuwa wapo kwa kurudi kwenye hip-hop.

Hatukuishia hapo tukakutana na shabiki mwingine ambaye yeye alikuwa tofauti kidogo kwani alienda kinyume na baadhi ya hao tuliotoka kupata mawazo yao, huyu yeye anafahamika kama John Mwalisanga anadai kuwa haoni kama kauli ya Khaligraph imeongeza chochote kwenye muziki huo badala yake msanii huyo wa Kenya amejiongeza umaarufu tu , kwani siku chache zilizopita Tanzania kulikuwa na session ya hip-hop ya free style ya Young Lunya na Young Killer, shabiki huyo akasema muziki huo upo mikono salama ya vijana wa Tanzania .

Aliendelea kwa kusema kuwa hip-hop haiwezi kufa wala kupotea kwani Amapiano ni muziki wa mpito tu kama ilivyokuwa kwa Kwaito ilikuja na ikapotea ndivyo pia itakuwa kwa Amapiano.

Hayo ni machache ya mashabiki wa muziki wa Hip-hop, kila mmoja ameweza kuzungumza lake, Khaligraph ameweza kuwaamsha na ameweka amsha amsha jamani hivyo basi mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, katika week hizi moto uliwaka sana huku mama  Omolo Rosa Ree akaachia ngoma kali mara kule Wakazi kazungumza lake mambo yalikuwa moto sana.

Mimi sina la ziada zaidi ya kusema na sign out tchaaao till next Friday, tutakutana hapahapa kwenye burudani zetu ni mwendo wa kuburudika tu na mambo yote ya kiburudani , tupate kupitia mitandao yetu ya kijamii kama mwananchi scoop, nawapentaaa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post