Gloritha Sulle: Mwanafunzi anayeagiza bidhaa nje ya nchi

Gloritha Sulle: Mwanafunzi anayeagiza bidhaa nje ya nchi

Na Aisha Lungato

Miaka ya hivi karibuni kumezuka biashara nyingi ambazo zinafanywa na watu wa kila rika na kila jinsia.

Licha ya kwamba biashara huwa haiaminiki lakini bado kuna watu wengi hawajakata tamaa, bado wanaendelea kupambana mpaka tone lao la mwisho, lengo ni kujiingizia kipato na kujikwamua kiuchumi.

Hata hivyo kwa sasa wasichana wengi wamekuwa wakifanya baishara ya kuagiza bidhaa mbalimbali za urembo, nguo, mshuka, vyombo nje ya nchi na kuleta hapa nchini.

Licha ya kuwa ni biashara ngumu lakini vijana wengi na mabinti wengi waliomo vyuoni na mtaani wameonekana kuipenda na kushawishika kuifanya.

Gloritha Sulle ni mmoja wa wajasirimali ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC).

Katika chuo hicho, Sulle anasomea kozi ya Journalism huku akifanya baishara hiyo ya kuagiza bidhaa nje ya nchi na kuuza katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Anasema kwa muda mrefu alitamani kufanya baishara yoyote ile kuepuka utegemezi kwa wazazi wake na kabla ya kuanza biashara aliomba ushauri kwa wafanyabiashara wengine.

Mbali na kufanya baishara hiyo Sulle ameamua pia kuuza vitenge na anaongeza kusema alifanya hivyo pia baada ya kupata ushauri kutoka kwa wafanyabishara mbalimbali juu ya aina ya baishara ya kuanza nayo.

“Mwanzo ni mgumu lakini wafanyabishara walionitangulia walinipa ushauri wa aina ya baishara ninayopaswa kuifanya ila mawazo yao niliyapokea lakini niliamua kuchagua mwenyewe biashara ninayotak akuifanya,” anasema

 KWANINI ULIAMUA KUFANYA BIASHARA HIYO

 “Niliamua kufanya biashara hiyo kwa sababu naipenda na kitu ambacho nimekuwa nacho,n nimekuwa nikiona mama yangu amekuwa akifanya biashara ya kuuza bidhaa mbalimbali  na mimi ikanipa hamasa ya kufanya biashara naweza kusema nikitu ambacho nimezaliwa nacho napenda sana kufanya biashara” amesema

Waswahili wanasema ukifanya biashara basi ukubaliane na yote na katika biashara kuna faida na hasara. Gloritha amefunguka kwa kusema

“Changamoto ninazo kumbana nazo ninyingi ukiwa unaagiza vitu nje ya nchi mfano unaweza kuagiza kitu kikaja tofauti na huwez kumrudishia  suppley huko aliko kwasababu tayari ni mbali pia changamoto nyingine ni mizigo kuchelewa ninacho shukru ni kwamba wateja wangu ni waelewa” amesema

Na kwa upande wa faida binti huyo amefunguka na kusema “ biashara ya mwanzo imeweza kuniletea biashara nyingine hiyo ni faida moja wapo pia kipato ninacho kipata kimewesa kunisukuma kimaisha na kufanya maendeleo yangu mengine” amesema

Ushari wako kwa  vijana wenzio walio mtaani na vyuoni, Sulle anasema “ ushauri wangu kwa vijana wawezs kutumia fursa zilizo mbele yao waweze kishuhurisha akili zao kiweza kutambua fursa zilozo mbele yao kwasasa kuota ajira ni ngumu kwahiyo kujiongeza kwao ndo kutawasaidia” amesema

Ukiwa kama mwanafunzi ukiachana na elimu yako na kozi unayo somea lazima kutakuwa na kitu ambacho huwa unakipemdelea zaidi vile vile kwa binti Gloritha kwa upande wake yeye anapendelea zaidi urembo na maswala mazima ya fashion kwa ujumala.

Kila binadamu ana ndoto zake yaani kuwa na matamanio kutaka kuja kuwa nani hapo baadae Gloritha yeye alifunguka kwa kusema kuwa

“Mimi natamani kuwa mfanyabiashara mkubwa ila kingine pia natamani siku moja nije kusaidia vijana ambao wanavipaji vyao hasa kwa wenye vipaji vya fashion maana kiko nyuma sana kuna watu wanawasaidia wanamuziki lakini kwenye maswala ya fashion yamesahaurika sana ni matumaini yangu siku moja ntakuja kufanya kitu kama hicho” amesema

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post