Gavana wa Japan, aitwaye Kengo Oishi ambaye alienda kumuona Cristiano Ronaldo akicheza katika mechi kati ya Al Nassr FC na PSG Julai 25, huku akiacha kuhudhuria mkutano wa magavana Japan atakwa kujiuzulu.
Gavana huyo Julai 25, aliacha mkutano wa magavana na kwenda kutazama mchezo huo na baadaye akashiriki katika hafla ya baada ya mchezo na nyota huyo wa Ureno Ronaldo jambo ambalo baadhi ya watu wamelichukulia kama matumizi mabaya ya madaraka.
Kutokana na kutakiwa kujiuzulu Gavana huyo ameendelea kujitetea kwa kudai kuwa alitumia pesa zake kununua 'tiketi' ya mechi hiyo, ingawa gharama za usafiri na malazi ziligharamiwa na serikali ya Mkoa. Pia amedai alitumia mkutano huo kumuomba Ronaldo kusaidia kulitangaza Jimbo la Nagasaki
Leave a Reply