Fahamu utundu wa Google chrome

Fahamu utundu wa Google chrome

Google Chrome ni kivinjari cha tovuti kilichotengenezwa na kampuni ya Google. Kivinjari hiki kilianza kutumika mwaka 2008 katika kompyuta za Microsoft Windows na baadae kufikia watumiaji wa programu endeshi za Linux, MacOS, iOS na Android. Kupitia makala hii utaweza kujifunza maujanja mbalimbali unayoweza kuyafanya katika kivinjari hiki.

Watu wengi wenye simu janja za Android au iOS hutumia kivinjari cha Google Chrome, leo kupitia kipengele cha smartphone tumewaandalia maujanja mbalimbali unayoweza kutumia ili kufurahia matumizi yako ya kivinjari hiki.

Kubadilisha Rangi ya muonekano wa kivinjari: Unaweza ukabadilisha muonekano mzima wa kivinjari hiki kwa kubadili rangi yake ya matumizi, ikiwa unaumia macho wakati unaitumia kutokana na muonekano wake mweupe basi unaweza kubadilisha na kuweka muonekano mweusi wa kivinjari chako. 

Kuchagua muda wa majibu yanayotokea kwenye kivinjari: Unapotafuta maudhui mtandaoni kupitia kivinjari hiki unaweza pia kuchagua muda wa matokeo ya maudhui utakayoletewa. Katika sehemu hii ya kuchagua muda utaweka tarehe, mwezi na mwaka wa kipindi cha muda unaopendelea na kuonyeshwa matokeo maudhui yake.

Kuwasha usalama wa maudhui kwenye kivinjari: Unapompa mtoto simu janja yako aperuzi mtandaoni unazuiaje aina ya maudhui anayoweza kuona mtandaoni? Katika kivinjari hiki cha Google Chrome kuna sehemu ya kuzuia maudhui hatarishi/ maovu.

Nikwambie tu kuwa kwa kawaida sehemu hii ya kuzuia maudhui hatarishi huwa imezimwa lakini unapoingia kwenye sehemu ya marekebisho ya kivinjari utaona kitufe cha kusogeza ili uweze kuwasha uwezo wa kivinjari kuchuja na kutoonyesha maudhui maovu kwa mtumiaji.

Kuona taarifa za ziada kuhusu tovuti unayotaka kutembelea: Kupitia kivinjari hiki utaweza kuona taarifa mbalimbali za ziada za tovuti unayotaka kuitembelea ikiwemo kama tovuti hiyo ni salama kufungua, wasifu wa tovuti hiyo na historia yako na tovuti hiyo kama uliwahi kuitembelea.

Dondoo hii imeandikwa kwa msaada wa Teknokona.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post