Fahamu kuhusu USSD CODE na mautundu yake

Fahamu kuhusu USSD CODE na mautundu yake

Habari mdau, karibu kwenye ukurasa wa Smartphone kama kawaida hapa utapata fursa ya kujifunza mambo kadha wa kadha yanayohusu teknolojia.

Leo moja kwa moja tutaenda kufahamu kuhusiana na Ussd code na maujanja yake karibu tujifunze kwa pamoja.

USSD Code ni itifaki ya mawasiliano inayotumiwa na simu za mkononi kuwasiliana na kompyuta za waendeshaji wa mtandao wa simu. USSD inaweza kutumika kwenye kivinjari kwa WAP, huduma za kulipia, huduma za pesa, huduma za maudhui kulingana na eneo, huduma za habari zinazotegemea menyu, na kama sehemu ya kusajili simu kwenye mtandao.

Katika matumizi yetu ya kawaida tumekuwa tukitumia sana hizi USSD Code kupitia mitandao mbalimbali ya simu kama Tigo, Vodacom, Airtel na Halotel. Leo tumekuandalia orodha ya USSD Code zitakazokuongezea maujanja ambazo ni hizi hapa:

Kupima hali ya simu: Unaweza kupima hali ya simu kwa kujaza tarakimu zifuatazo (*#0*#), ambapo utaonyeshwa menyu ya kuchagua ni uwezo upi wa simu janja yako unaotaka kuupima. 

Kuangalia IMEI namba ya simu: Endapo utahitaji kujua IMEI namba ya simu janja yako unaweza kuiangalia kwa kubofya tarakimu zifuatazo kwenye simu janja yako (*#06#). Baada ya kuona IMEI namba yako unaweza kuirekodi pembeni kwaajili ya matumizi ya baadae.

Kuangalia kama simu yako inasikilizwa: Unapokuwa na mashaka yoyote kuhusu simu yako kusikilizwa au ujumbe kusomwa na mtu mwingine unaweza kutumia tarakimu hizi kuchunguza hali hii (*#67#). Kupitia njia hii utaweza kuona kama maongezi yako yanasikilizwa au jumbe zako zinasomwa. Pia ukitaka kuona ni namba gani ya simu inasikiliza au kusoma jumbe zako utatumia tarakimu (*#61#).

Kuficha uwepo wako kwenye programu za Caller ID: Kujali faragha yako ni jambo la msingi hivyo kutokana na watu wengi kutumia programu za Caller ID siku hizi unaweza kutumia tarakimu zifuatazo (#31#) kuzuia mtu kukutambua kupitia programu hizo.  Kwa orodha ya USSD Code zingine tembelea tovuti hii.

Dondoo hii imeandikwa kwa msaada wa wesite ya tekno kona.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post