Niaje mwanangu mwenyeweee!! Aaah wewe hatari kabisa leo ndani ya smartphone bwana nakuletea njia ambazo ni rahisi kuzitumia pindi betri ya simu yako ikiwa mpya ili lisiwahi kuharibika unazijua ni zipi hizo? Twende sawa sasa.
Hii imeshatokea bwana, watu wengi wamekuwa hawafahamu wafanyaje ili kutunza betri la simu ambalo ni jipya ili lisiwahi kuharibika.
Ukiwa na wewe ni miongoni katika hao basi usivurugwe mambo mapesi kabisa ungana nami leo nitakueleza namna ya kuchaji betri likiwa jipya ili lisiharibike mapema twenzetuu!.
Sasa basi, mara tu baada ya kununu simu, Iwashe simu hiyo kisha angalia ina asilimia ngapi ya chaji, Baada ya kuona ina asilimia ngapi, unashauriwa kufanya yafutayo;
Kama ina asilimia hamsini (50%) au zaidi usiweke simu kwenye chaji bali unatakiwa kuitumia, mpaka chaji hiyo itakofika asilimia kumi (10%) ndipo uiweke kwenye chaji.
Baada ya kuweka kwenye chaji hakikisha unaichaji simu hiyo kwa muda wa masaa matatu ndipo uanze kuitumia tena, Kwani baada ya masaa matatu itakuwa imejaa vizuri kwa ajili ya matumizi sasa.
Lakini endapo umenunua simu mpya au betri jipya mara tu baada ya kuwasha ukakuta ina chaji ambayo ina asilimia arobaini na tisa (49%) kushukua chini (49%-0%) tafadhali sana mtu wangu! usiitumie simu au betri hilo, bali iweke chaji kwa muda wa masaa matatu ndipo uanze kuitumia simu hiyo.
Jambo la muhimu na lakuzingatia ni kwamba, kumbuka kuichaji simu yako kila wakati, kila inafika chaji kwa kiwango cha asilimia kumi (10%)
Kufanya hivi kutakusaidia sana kuweza kulitunza betri lisiharibike mapema nadhani umenipata vyeemaaa kabisa, this is Smartphone Mwananchi Scoop tunakwambia enjoy your Smartphone page every wednesday of the week hollaaaa!!!
Leave a Reply