Fahamu kuhusu biashara ya kurejea chupa (Recycling)

Fahamu kuhusu biashara ya kurejea chupa (Recycling)

 

Mambo vipi? Its another week kwenye chimbo letu la biashara ndani ya Mwananchi Scoop, kama kawaida na kusogezea fursa mbalimbali kuhusiana na biashara na lengo kujifunza kwa kujua faida na changamoto zake lakini pia kujiari.

Ebwana hivi ushawahi kuwaza au kufikiria kuhusu kuanzisha biashara ya kuokota chupa? Je jamii inawachukulia vipi wale ndugu zetu wanaojitafutia tonge kwa kuokota chupa mtaani? Pia ushawahi jiuliza zile chupa hupelekwa wapi? Basi katika biashara week hii utaweza kufahamu  kuhusu biashara ya kurejeleza chupa (recycling).

Kurejeleza chupa (recycling) ni mbinu ya kuziokota chupa zilizotumika au takataka ambazo kwa kawaida haziwezi kutumiwa tena  na kuirejeleza kwa matumizi mazuri ya malighafi ili
kukua kiuchumi.





Mfano wa chupa ambazo zinazoweza kufanyiwa recycling kama;

  • Chupa ya kioo iliyotumiwa na kuvunjika, urejelezaji hufanyika kwa kuyeyusha kioo upya na kutengeneza chupa tena.
  • Chupa za plastiki ambazo hizi huokotwa kwa wingi mtaani ikiwa pamoja na vifuniko vya chupa, mifuko ya plastiki kutokana na uhitaji wa kiwanda husika kinachofanya mchakato huo.

Vilevile aina zingine za urejelezaji takataka unaweza kuwa wa karatasi za magazeti au vitabu zinaweza kutibiwa kuwa karatasi mpya

  • Vifaa vyote vya metali kama motokaa vilivyoharibika vinaweza kutumiwa kutengeneza chuma.
  • Takataka ya vyakula au majani vikifanyiwa mchakato wa urejeleshi huwa mbolea katika kilimo au bustani.
  • Nguo zilizoharibika zinaweza kukatwa na kutumiwa kwa kutengeneza uzi mpya.

 

 

 

 

Alama ya urejelezaji

 FAIDA YA UREJELEZAJI CHUPA ZA PLASTIKI

  • Husaidia kuhifadhi mazingira kwa kupunguza uzagaaji wa takataka.
  • Unapunguza gharama za vitu kwa kutunza thamani iliyobaki katika takataka.
  • Husaidia watu kupata ajira kwa kuokota na kuuza chupa kiwandani vilevile watu kupata ajira kiwandani katika kusimamia vitendea kazi kukamilisha mchakato huo. 
  • Pia huongezea pato katika taifa kwa kulipa kodi kupitia wawekezaji wanaofungua au kuanzisha viwanda vinavyohusika na urejelezaji.

 

NAMNA YA UKUSANYAJI MALIGHAFI

Wamiliki wa viwanda ambao ndo wanunuzi wa chupa kwa ajili ya kufanya urejelezaji hutumia mawakala wa mtaani ambao hununua chupa kwa watu na kuzikusanya katika uzito wa kilogramu tofauti na kuzipeleka kiwandani ambapo mtaani kilo1 ya mzigo wa chupa hununuliwa kwa shilingi 1000/=

Vilevile bei ya ununuzi wa mzigo wa chupa kutoka kwa wakala kwenda kiwandani hutegemea na kiwanda husika maana hutofautiana bei kulingana na aina ya malighafi ya chupa.

BIDHAA ZITOKANAZO NA UREJELEZAJI WA CHUPA

Katika urejelezaji wa chupa viwanda vingi huyeyusha chupa ili kutengeneza chupa mpya na viwanda vingine hukata chupa hizo katika vipande vidogo vidogo na kusafirisha nje ya nchi kama Ujerumani, Dubai, Afrika ya Kusini na China kwa lengo la kutengeneza bidhaa zingine, miongoni mwa bidhaa zitokanazo na  urejelezaji ni;

  • Viti vya plastiki
  • Midoli ya watoto
  • Mapambo ya ndani kama maua nk
  • Viatu
  • Kamba na nguo.

CHANGAMOTO YA BIASHARA YA UREJELEZAJI WA CHUPA.

Baadhi ya wafanyabiashara wa urejelezaji wa chupa wamefunguka na kusema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni miongozo ya kanuni na sheria kutokuwa rafiki ili kuwafanya biashara yao kuwa endelevu pia kuweza kuwakaribisha wawekezaji ili kukuza biashara hiyo.

Vilevile vibali vinavyowaruhusu kufanya biashara hiyo vimekuwa vingi kulinganisha na mtaji au faida itokanayo na biashara hiyo.

Mwanangu wa faida amka kila kitu ni mchongo inategemea na ubunifu wako katika kuifanya iwe pesa, nani aliyefikiri kama takataka tena machupa yanaweza kutengenezewa kitu kingine kipya chenye thamani? Tukutane wiki ijayo katika kona hii hii ya biashara ndani ya mwananchi scoop.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post