Baada ya jana mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube kufuta utambulisho na picha zote alizopiga akiwa na jezi za timu hiyo, leo ameendeleza kuonyesha kuwa haitaki tena timu hiyo licha ya kuwa ana mkataba wa miaka miwili na nusu kama klabu hivyo inavyodai.
Kupitia akaunti yake ya Instagram #Dube ameposti barua yenye ujumbe wa kuishukuru klabu hiyo, vingozi, ‘benchi’ la ufundi pamoja na wachezaji wenzake hivyo angependa kufungua ukurasa mwingine wa maisha yake ya ‘soka’.
#Dube aliandika barua kuondoka Azam na kupewa masharti ya kufuata utaratibu wa kuvunja mkataba, licha ya kuwa hakuweza kuyafuata.
Ili kuvunja mkataba #Dube, anatakiwa kuilipa #Azam dola 300,000 ikiwa ni zaidi ya Sh750 milioni ambapo taarifa zinadai kuwa nyota huyo alipeleka nusu ya pesa na Azam walizikataa kwani anatakiwa kulipa zote kwa wakati mmoja.
.
Leave a Reply