Mfanyabiashara na mkali wa Hip-hop Marekani Diddy Combs ameripotiwa kuuza jumba lake la kifahari lililopo jijini Los Angles kwa dola milioni 70 ikiwa ni sawa na Sh 185.8 bilioni.
Uamuzi huu unakuja miezi minne tu baada ya nyumba zake mbili kuvamiwa na Idara ya Usalama Marekani kuhusiana na kesi ya kutuhumiwa kujihusisha na biashara ya ngono.
Chanzo cha karibu cha ‘rapa’ huyo kilizungumza na TMZ kilieleza kuwa Combs alifanya uamuzi wa kuuza nyumba hiyo kwa lengo la kuondoka kabisa jijini Los Angeles huku wiki tatu zilizopita akionekana kwenye nyumba yake ya West Hollywood iliyopo Miami.
Ikumbukwe kuwa Machi 25, 2024 makazi ya nyota wa muziki wa hip-hop, Sean "Diddy" Combs, ya Los Angeles na Miami yalifanyiwa upekuzi na Mawakala wa Usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo.
Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za biashara ya ngono na unyanyasaji wa kijinsia tangu Novemba mwaka jana huku aliyekuwa mtayarishaji wa kazi zake Rodney "Lil Rod" Jones akidai kuwa Combs alikuwa akiandaa sherehe za biashara ya ngono.
Aidha licha ya kufunguliwa kesi nane moja ikiwa ya siku mbili zilizopita, lakini bado hakuna ushahidi madhubuti wa kumtia nguvuni mwanamuziki huyo huku baadhi ya mastaa akiwemo Suge Knight wakidai kuwa Diddy ni FBI.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply