Dhana ya uhaba wa wanaume huwaweka baadhi ya wanawake katika mahusiano magumu

Dhana ya uhaba wa wanaume huwaweka baadhi ya wanawake katika mahusiano magumu

Kuna wakati hutokea wanawake wakateswa sana kwenye uhusiano wao wa kindoa au kimapenzi na bado wakaendelea kukaa tu kwenye uhusiano huo.

Inafikia hadi mtu anakufa huku akiona kabisa. Watu wengine huiita hali hii kuwa ni ujinga na wengine huita kulogwa au huelezea hali hii kwa njia ambayo haiwapi haki wanawake hao.

Zipo sababu nyingi ambazo zinawafanya wanawake kuendelea kukaa kwenye mahusiano magumu au ndoa ngumu, bila hata kufikiria kuondoka.

Sababu nyingine zinaweza kuonekana kama kituko, lakini ndizo zinazowafanya wang’ang’anie uhusiano huo au wafie kwenye uhusiano au ndoa hiyo.

Kuna dhana imejengeke kwa baadhi ya wanawake kwamba wanaume ni wachache au hakuna wanaume wa kuoa. Dhana hii ambayo haina ukweli wowote, imewafanya baadhi ya wanawake kuishi katika mahusiano magumu na wenzi wao wakihofia kutoka au kuachana nao kwa sababu hawatapata mwanaume mwingine.

Kuna wanawake wengi sana ambao wanagombea kupendwa, au wanajipendekeza ili wapendwe. Hawa ni wanawake ambao wana kasoro kubwa kwenye mifumo yao ya kufikiri au ufahamu.

Unaweza kukuta mwanamke anadhalilishwa, anaoneshwa kwamba hatakiwi, amechokwa, ameshachezewa lakini amemng’ang’ania mwanaume huyo kama luba.

Wanawake wanaoteswa kwenye uhusiano au ndoa, huwa wanajidanganya kwamba, watamudu siku moja kubadili tabia hiyo a waume zao kuwafuja.

Wanajiambia kwamba, kutukanwa, kupigwa, kudhalilishwa, na matendo mengine, kuna siku watamudu kuwasaidia wanaume hao watoke kwenye tabia hizo.

Lakini wakati mwingine wanaume hawa watesaji, huwa wanajidai kusema kwamba, wanafanya mambo hayo bila kujua sababu na kuna wakati wanasema wamelogwa.

Hujawahi kuwaona wanawake wanaokwenda kwa waganga kutafuta dawa ili waume zao wasiwapige, ati kwa sababu vipigo vyao vinatokana na kuchanganywa na uchawi wanaofanyiwa na wanawake zao wa nje? Mwanamke anaamini kabisa kwamba, mumewe hamjali na anamdhalilisha kwa sababu ya kulogwa!

Mwanamke anaweza kujiambia kwamba, kwa sababu mume wake kuna wakati anamtendea wema, hata kama ni mara moja, basi anampenda na hayo mengine mabaya, yatakwisha au ni bahati mbaya.

Mwanamke pia anaweza kufikiri kwamba, akijitahidi sana kumfurahisha mumewe, mume huyo atabadilka na kuwa na tabia nzuri. Hivyo hujipendekeza na mwanaume habadiliki na mateso yanaongezeka.

Kuna wanaomudu kutoka kwenye uhusiano wa aina hiyo, hawa ni wale ambao wanajua nini maana ya kupenda wao hawasukumwi na mihemko, bali husukumwa na kupenda. Kwao msamiati kwamba wanaume ni wachache au hakuna wanaume wa kuoa haupo kabisa akilini mwao..............

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Shaban Kaluse

A Sales and Marketing in the hospitality Industry and also a freelance journalist, writing about love and relationships and educative articles which aims for youths, every Tuesday on Mwananchi Scoop.


Latest Post