BASATA yalaani tukio la Zuchu kurushiwa vitu jukwaani

BASATA yalaani tukio la Zuchu kurushiwa vitu jukwaani

Baraza la Sanaa la Taifa 'BASATA' limelaani vikali tukio lililotokea Septemba 28, mkoani Mbeya la mwanamuziki Zuhura Othman Soud 'Zuchu' kurushiwa vitu jukwaani wakati akitumbuiza.

Kupitia taarifa iliyotolewa na BASATA leo Oktoba Mosi, imewataka wadau wa sanaa na wasanii kuheshimu misingi ya kiungwana ili kuepusha migongano isiyo na tija. Pamoja na hayo, waandaaji wa matukio wametakiwa kuzingatia uwepo wa mazingira salama kwa wasani na wadau wake wakiwa katika majukumu yao.


"Kwa mujibu wa Kanuni ya 50 (1) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018 inatoa mamlaka kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuwa mratibu wa matukio yote shughuli za sanaa chini yakizingatia misingi ya kizalendo, kiungwana, utu na mshikamano.

"Kutokana na hilo, Baraza la Sanaa la Taifa linalaani tukio lililovuruga utumbuizaji kwa mwanamuziki Zuhura Othman Soud (Zuchu) baada ya kutupiwa vitu jukwaani na mashabiki wasiokuwa waaminifu katika tamasha la Wasafi Festival, tarehe 28 Septemba 2024, lililofanyika Mkoani Mbeya,"imeeleza taarifa hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post