Baada ya zaidi ya video 300 za ngono kusambaa katika mitandao ya kijamii za Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha (ANIF) kutoka Guinea ya Ikweta Baltasar Engonga, na sasa anafananishwa na mkali wa Hip hop wa Marekani Diddy.
Kufuatia na video hizo ambazo zinaendelea kuzuliwa ili zisisambae, zikimuonesha Mkurugenzi huyo akijihusisha na videndo vya kingono baadhi ya mashabiki kutoka sehemu mbalimbali kwenye mitandao wameifananisha kesi yake na ya rapa Diddy.
Utakumbuka Diddy alikamatwa na kutupwa gerezani Septemba 16 jijini Ney York kwa makosa makubwa ya unyanyasaji wa ngono huku kesi yake ikianza kusikilizwa Me 5, 2025.
Aidha katika mitandao mbalimbali wadau wameandika, Salome kipenzi “Diddy wa Africa” , huku kupitia mtandao wa Threds anayefahamika kwa jina la Nteziryayo Le Rwandais akiandika “Kutana na P.Diddy wa Malabo, Baltasar Ebang Engonga. Yeye ndiye mkuu wa Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Kifedha la Guinea ya Ikweta”
Engonga anashikiliwa na polisi kufuatia na uchunguzi wa madai ya ufisadi na udanganyifu, ambapo video hizo zilikutwa nyumbani kwake baada ya maafisa wa polisi kufanya upekuzi katika nyumba yake.
Mamlaka zilipata kanda kadhaa zenye video za wanawake hao zaidi ya 400, wakiwemo wake za viongozi, mke wa mchungaji wa Engonga, jamaa wa rais wa nchi hiyo, na wake za mawaziri zaidi ya 20.
Leave a Reply