Davido aitwa mnafiki baada ya kupiga kura Marekani

Davido aitwa mnafiki baada ya kupiga kura Marekani

Mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, Davido ameitwa mnafiki na baadhi ya mashabiki wa Nigeria baada ya kutangaza kupiga kura kwa mara ya kwanza katika nchi anayoishi.

Kupitia ukurasa wake wa X Davido alishare picha yake akiwa ameshika stika iliyoandikwa ‘Nimepiga Kura’ jambo ambalo liliwaibua mashabiki katika upande wa komenti huku wakimnanga kuwa kwanini hakutoa sauti kwenye uchaguzi wa Nigeria wa mwaka 2023.

“Mtu huyu ni mnafiki, hujawai kupiga kura katika uchaguzi wowote wa urais nchini Nigeria, lakini sasa unatafuta kuthibitishwa na Wamarekani," alikomenti shabiki mmoja.

Mbali na huyo naye mwanamitandao kutoka nchini humo Daniel Regha aliyatoa ya moyoni kwa kumtaka Davido aache kujivunia kupiga kura Marekani.

"Davido, hii nguvu ilikuwa wapi wakati wa uchaguzi mkuu wa Nigeria? Haukuonyesha ushahidi wa kupiga kura, haukuonyesha msaada kwa wapiga kura, wala hata kujitahidi kutumia jukwaa lako kuuita INEC wakati kulikuwa na ripoti za udanganyifu wa uchaguzi kote nchini. Lakini sasa unajivunia kupiga kura kwenye uchaguzi wa Marekani? Hii siyo mafanikio unayofikiri niyo."

Hata hivyi baadhi yao walimuonya mkali huyo wa Afrobeat kwani kujiweka karibu sana na Wamerekani hakutaomfanya kuonekana bora zaidi kwa wasanii wa Marekani bali ni kuidharirisha nchi yake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags