Hali ya hewa yakwamisha Davido kuchangia jukwaa na Diamond

Hali ya hewa yakwamisha Davido kuchangia jukwaa na Diamond

Mwanamuziki kutoka Nigeria Davido ametangaza kutokuwepo kwenye usiku wa Tuzo za Earth Prize zinazotarajiwa kufanyika leo Capetown nchini Africa Kusini, huku akitaja sababu kuwa ni hali mbaya ya hewa nchini Marekani.

Davido ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram akieleza kuwa yeye na team yake wamefanya jitihada ili waweze kufika lakini haikuwezekana.

“Nasikitika kutoweza kutumbuiza kwenye Earthshotprize Cape Town kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya,tumejaribu kila kila liwezekanalo lakini muda haukuwa upande wetu nawatakia kila la heri”

Aidha katika tuzo hizo Davido alitakiwa kushare steji na wasanii wenzake akiwemo Diamond kutoka Tanzania, Uncle Waffles wa Afrika Kusini na wengineo.

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho Davido na Diamond kutumbuiza katika jukwaa moja ilikuwa ni kwenye tamasha la ugawaji wa tuzo za ‘Trace Music Award’ zilizofanyika nchini Rwanda mwaka 2023.

Davido amekuwa bize kwa takribani wiki sasa, ambapo wikiendi iliyoisha alionekana katika sherehe ya kutimiza miaka 40 ya mwanamuziki Angélique Kidjo iliyofanyika jijini New York huku jana akishiriki kwenye zoezi la upigaji kura nchini humo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags