Baadhi ya mastaa walio fariki, Wanaishi kupitia mitandao ya kijamii

Baadhi ya mastaa walio fariki, Wanaishi kupitia mitandao ya kijamii

Kumekuwa na utofauti mkubwa sana kwa watu wanao julikana nchini, hasa likija suala la kuwakumbuka. Watu maarufu Bongo wakipoteza maisha basi kama ni mwanamuziki atakumbukwa kwa nyimbo zake tu, kama muigizai basi wachache wakiona movie zake ndipo humkumbuka mtu huyo.

Lakini kwenye upande wa kuwakumbusha watu kuwa aliwahi kuwepo mtu fulani maarufu kwenye mitandao ya kijamii, huwa linaishia tu mara baada ya mtu huyo kufariki.

Jambo hilo ni tofauti kwa baadhi ya watu maarufu kutoka nchi nyingine ambao walikuwa wakitumia mitandao ya kijamii lakini hata baada ya kufariki bado wanaendelea kukumbukwa kupitia mitandao hiyo.

Kwani page zao bado zipo active zinafanya kazi kama kawaida, kwa kuendeshwa na watu wa karibu wa marehemu hao.

Mfano mzuri unajionesha kwa watu kama Costa Tich ambaye hadi sasa account yake ya Instagram bado ipo active inaendeshwa na mama yake mzazi, 2Pac naye tunaona mambo ni moto inaendeshwa na Shakur Estate, AKA account yake inaendelea kufanya vizuri ikishikiriwa  na management yake pamoja na The Forbes family.

Chadwick Boseman ambaye wengi mlimuona kupitia filamu ya Wakanda Forever pia ukurasa wake wa Instagram bado upo macho mikononi mwa Team CB, bila kumsahau Michael Jackson naye yupo active Instagram.

Aliyekuwa mkali wa Fast and Furious Paul Walker bado tupo naye kihisia kupitia #Instagram yake, upande wa soka unamkuta mkali wa kuutuliza mpira Pele bado account yake ya Instagram inafanya vizuri.

Hao ni kati ya wakali ambao walifariki miaka tofauti tofauti bado wanaishi katika vichwa vya mashabiki kupitia mitan






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post