AIDU ZUBERI: Kijana anayejituma kwenye football

AIDU ZUBERI: Kijana anayejituma kwenye football

Aiseee, kwenye haya maisha bwana kila mtu ana jambo ambalo linamchukiza na hatamani haswa, aidha kufanyiwa yeye binafsi au kuona mtu mwingine anafanyiwa katika jamii, sijui unanipata hapo?

Aidu Zuberi ni mwanafunzi kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) akiwa anasomea Bachelor of Arts in Education.

Aidu ni kijana mwenye kipaji kikubwa sana cha kucheza mpira wa miguu lakini kwenye safari ya maisha yake ana ainisha jambo ambalo hapendi kufanyiwa au kuona mtu mwingine anafanyiwa.

“Kitu nisichopenda kufanya au kufanyiwa, sipendi unafiki nachukia sana mtu akiwa mnafiki kwenye jamii au kuna ile mtu  suala zima la kuanzisha ugomvi au malumbano,” anasema.

Akizungumza na jarida la Mwananchi Scoop, Aidu amesema kuwa football ndio mchezo pekee anaoukubali na kuuelewa sana kwenye maisha yake.

“Football ndio mchezo ambao ninaoumudu sana na unanipa furaha siwezi kupitisha siku bila kucheza mpira au hata kuangalia, kiukweli nina malengo nao mchezo huu.”

Kwa nini football na sio basketball ama mchezo mwingine?

Sio basketball kwasababu hata height yangu hairuhusu kwani kwenye basketball mara nyingi wanachukua watu warefu zaidi. Binafsi the way nilivyo nafiti sana kwenye mpira wa miguu lakini pia basketball is not my choice,” anasema.

 

Je mpira umeuchagua kua ndiyo mbadala wa course yako?

Ndio. Mpira nimeuchagua kuwa mbadala wa course yangu kwa sababu ndoto yangu kubwa sana ni kuja kuwa mchezaji mkubwa hapa nchini,” anaongeza.

Why vijana wengi wanashabikia mpira wa miguu?!

Aidu anasema, “Vijana wengi wanapenda mpira wa miguu na kuushangilia kwasababu mpira unatufanya vijana kuwa na muunganiko, kuwa na umoja ndiyo maana utakuta vijana wanaungana kwenye mechi zozote zile.”

Je una malengo ya kuja kucheza soka la aina gani?

“Malengo yangu mimi ni kuja kucheza soka la kulipwa, iwe ndani ya Tanzania au nje ya nchi au hata Afrika kwa ujumla, hilo ndilo lengo langu,” anaongeza.

Changamoto unazokutana nazo?

“Changamoto kubwa ninazokumbana nazo ni za nje ya uwanja nakosa support kwa watu unajua tunacheza mpira lakini ndoto zetu haziwezi kukamilika bila kupata support yoyote ile na watu ambao wapo tayari kwenye system za mpira wa miguu hiyo ndo changamoto niliyonayo,” anasema.

Je mpira hadi sasa umekunufaisha chochote?

“Kwa level yangu niliyokua nayo naweza kusema kuwa mpira umeninufaisha, nimebahatika kwenda mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, nilikua sipafahamu lakini mpira ndio umenipeleka huko,” anasema na kuongeza,

“Lakini suala jengine ni kupata connection za watu mbalimbali ikiwemo wachezaji wenzangu kutoka vyuo vyengine hayo nayo ni mafanikio ambayo naweza kusema nimeyapata”

Owkey kama kijana kipaumbele chako ni kipi?

“Kama kijana kipaumbele changu kikubwa ni kufanya kazi kwa juhudi na kujitoa napenda hata vijana wenzangu wafanye haya kwasababu umri unakwenda hivyo tukifanya kazi kwa juhudi tunaweza kufikia malengo yetu’ anasema.

Je wewe unapenda nini ?

“Napenda amani na upendo mimi ni mtu wa hivyo kabisa yaani napenda kama sisi vijana tupendane kila kijana ampende mwenzie hii itatusaidia katika kufikia malengo yetu”

“Mara nyingi unakuta kijana mwenzio anamchongo wa maana kabisa lakini kwasababu mnakunjiana kila siku hawezi kukupa hivyo unawza kujikosesha mambo yako ya msingi kwenye maisha kwa sababu ya mambo kama hayo”

“kwenye hili nasisitiza sana vijana tubebane tushikane tupeane mawazo ukimuona mwenzio hayuko vizuri hata darasani msaidie mshauri tumetoka kwenye mazingira tofauti sana katika jamii kuharibikiwa kwa kijana mwenzio sio fahari kabisa”anasema

Kitu gani kina kupa amani?!

Kiukweli kitu ambacho kinanipa amani na faraja kwenye maisha yangu ni kuona familia inayonizunguka tupo kwenye amani na upendo hivi vitu kiukweli kwangu vina thamani kubwa mnoo nalilia hili kila siku kwakweli”anasema

Mchezaji gani unamkubali kibongobongo?

“Kibongo bongo mchezaji ambaye namkubali sana na napenda kumuangalia ni Luis Mixon kutoka Simba ni mchezaji ambaye anajituma na nakuwa serious sana akiwa uwanjani ndiyo ninaemkubali na ni role model wangu,” anasema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post