Naam its Friday, kama kawaida karibu sana kwenye kipengele chetu cha makala za burudani ambapo hapa huwa tunakuletea taarifa kadha wa kadha zinazohusu mastaa wakubwa bila kuwasahau wale ambao ni chipukizi.
Yap wiki hii nimekuletea vijana makini kabisaa, bila shaka kama wewe ni mfuatiliaji wa masuala ya burudani basi utakua unawafahamu fika kabisa vijana hawa, si wageni bali nawatambulisha kwako ‘Buza Kwaya’.
Buza Kwaya bhana ni vijana wawili ambao wamejipatia umaarufu mkubwa hususani kwenye mitandao ya kijamii yaani Instagram, TikTok pamoja na YouTube kutokana na kazi ambazo wanazifanya.
Hawa ni vijana ambao wameamua kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa mtindo wa uimbaji wa kwaya ambao umewavutia na kupendwa na watu wengi.
Vijana hawa mara nyingi huchukua muziki ama nyimbo za bongo fleva na kuzipeleka kwenye mtindo au ladha ya kwaya, tunaweza kusema hivyo na ukapata ujumbe kama kawaida kwa njia hiyo ambayo ni ubunifu mkubwa ambao wanaofanya.
Buza Kwaya inawahusisha vijana wawili akiwemo Nathan Ishengoma pamoja na Adrat Jacob ambao wameungana kwa pamoja kwa ajili ya kufanya kazi yao ya sanaa.
Aidha vijana hawa wamepata umaarufu mkubwa sana kupitia clip ya wimbo wa Diamond Platnumz ‘Iyo’ iliwatambulisha kwa hadhira na kuweza kupata interviews mbalimbali na kupata kazi za kufanya kwenye hafla kadha wa kadha.
Hata hivyo tayari wameshaanda project yao ambayo itakwenda tofauti na vile ambavyo watu wamezoea.
“Sisi kama Buza Kwaya, project yetu inayokuja tumepanga kubadilisha namna ya uimbaji ambao tunaimba kwa namna nyingine tofauti lakini kazi zitabaki kuwa vilevile nyimbo za bongofleva tunabadilisha katika miondoko ya dini,” Buza Kwaya.
“Tulikua na namna moja ambayo tumezoeleka sana sasa hivi project tutakayofanya ni kubadilisha ile aina ya miondoko siwezi kuiweka bayana coz ni surprise kwa mashabiki zetu.”
Sambamba na hayo Buza Kwaya kupitia kazi zao ambazo wamezifanya tayari wamebahatika kupata tuzo moja ambayo walikabidhiwa na Rais wa Chuo kikuu cha Dar es salaam, ndugu Spenser Minja ambaye aliandaa tuzo hizo zilizotambulika kwa jina la Presidential Honorary medal.
Tuzo hizo zikiwa na lengo la kuwapongeza watu wanaofanya vizuri ambapo Buza Kwaya walikabidhiwa kupitia kipengele cha Entertainers na kupata medal pamoja na cheti.
Mafanikio yao
Kupitia mohijiano yaliyofanyika na jarida la Mwananchi Scoop vijana hao walisema kuwa wanajivunia sana tuzo ambayo walikabidhiwa na Rais wa Chuo cha UDSM kutokana na aliweza kuheshimu uwepo wao kwani watu wa nje waliona lakini hawakuweza kuwapongeza kwa kile walichokifanya.
Changamoto za kazi
Vijana hawa walifunguka jinsi gani wanaumia na mapokeo ya baadhi ya watu ambao wanamitazamo tofauti na kazi ambayo wanaifanya.
“Kiukweli tunaumizwa sana tu na watu ambao hawakubaliani na kitu ambacho tunafanya hususani kwa watu ambao wana Imani kali kwenye masuala ya dini ambao wanaona kama tunaidhihaki yaani tunakwenda kinyume na matakwa ya Mungu.”
“Sisi pia ni wakristo tunaamini, tunasali lakini hiyo ni changamoto ambayo inatuumiza sana hua tunafikiria kuacha lakini tunapiga moyo konde kwani Mungu ndiyo anaetoa vipaji kwani nasi tunakitumia kama mtaji ili kuendeleza maisha yetu.”
Matamanio yao
“Buza kwaya sisi tunatamani sana kufikia hatua ambayo kila mmoja atatambua nini ambacho tunafanya, lakini pia tuweze kupata mialiko mbalimbali ya kuperform show kubwa ziwe ndogo tu kama hizi za vyuoni ambazo tumezoea kuzifanya”
Hitoria yao namna walivyoanza kazi ya ucheshi
“Kiukweli historia yetu tumekutana katika shule ya Kibiti Boys pwani ambapo ndipo ilipoanza safari ya kukutana kwao, na kufanikiwa kusoma mchepuo mmoja wa HGL.”
“Safari yetu ya Ucheshi rasmi ilianza Chuo mwaka wa kwnza kwani tulipangiwa hostel moja na chumba kimoja, ambapo hapo ndipo tulipoanzia tukiwa tunafanya clip za kawaida tu za kuchekesha”
Msichokijua kuhusiana na Buza Kwaya
“Sisi tumeishi mpaka hatua hii tunakaribia kuwa ndugu lakini hapo mwanzo katika shule ambayo tumesoma pamoja tulikuwa hatujawahi kuwa marafiki hata kidogo wala kushare vitu tunavyovifanya”
“Sisi huwa tunagombana sana wakati wa kuandaa hizi kazi inafika hatua ya kila mmoja anasusa kabisaa, lakini baadaye tunapata tunafanya tena kwani tunamuungano ambao uko imara sana”.
Kitu gani mnataka watu wafahamu kuhusu ninyi?
“Sisi bwana ni wasanii tumesoma na tuna degree ya Sanaa kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, tunaamini Sanaa sio uhuni kwani ni chanzo cha kipato kutokana na watu wanaweza kujiajiri kupitia sanaaa.
Leave a Reply