Wahitimu NIT washauriwa kutengeneza ajira, kujiajiri

Wahitimu NIT washauriwa kutengeneza ajira, kujiajiri

Katika kuhakikisha kunakuwepo na ongezeko kubwa la watu wanaojiajiri, Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wameshauriwa kutumia ubunifu na maarifa waliyoyapata kutengeneza ajira, kujiajiri sio kutegemea kuajiriwa pekee.

 Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Abdi Mkeyenge wakati wa maadhimisho ya Kongamano la nane la Wahitimu wa Chuo hicho cha NIT.

Katika kogamnao hilo NIT ilibainisha malengo yake ya ushindani katika kuwandaa wanafunzi wenye ujuzi na ubunifu watakaoweza kutengeneza ajira kupitia fursa ambazo Serikali imezitangaza ikiwemo uchumi wa Buluu, ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga Tanzania.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mkeyenge amesema ubunifu na maarifa wanayopatiwa wanafunzi wa NIT wanapaswa kutokaa nayo badala yake watumie kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

“Tuache kabisa dhana ya kuajiriwa bali tufikilie zaidi kujiajiri, najua ujuzi, maarifa na tafiti mlizozipata hapa chuoni ni nyenzo kubwa kwetu katika kutengeneza jira, zinduka sasa na chukua hatua ya kujiajiri pale unapoona fursa ya kufanya hivyo,” amesema

Awali akizungumza katika Kongamano hilo Mkuu wa Chuo cha NIT, Profesa Zacharia Mganilwa amesema kongamano hilo limelenga kuwakutanisha walimu, wanafunzi na wahitimu kwa kuwaonesha dira baada ya kuhitimu na namna ya kutumia maarifa waliyoyapata kwa vitendo kwa kujitengenezea ajira zao na kuajiri wengine.

Amesema chuo hicho kimejikita katika ushindani hasa kwa wakati huu ambao dunia ipo katika mageuzi makubwa ya kiuchumi na fursa nyingi katika sekta ya usafirishaji.

"NIT imekuwa ikiongeza ufanisi na kufanya tafiti mbalimbali ambazo zimekiwa zikiinua chuo hiki kwa kufanya vizuri wakati huu ambao ulimwengu unashuhudia mapinduzi makubwa ya teknolojia.'' amesema.

Mganilwa amesema Kongamano hilo linawaweka pamoja wanafunzi, walimu na wahitimu na kujadili mabadiliko yenye tija kwa jamii pamoja pamoja na kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao.

Pia linatumika kutoa zawadi kwa wastaafu waliotumikia chuo hicho kwa miaka 30 pamoja na kutoa zawadi kwa wakufunzi waliopata mafunzo ndani na nje ya nchi.

Aidha amesema katika kongamano hilo chuo hicho kimesaini hati ya makubaliano na kampuni ya Simba Logistics ambao ni wadau wakubwa wa usafirishaji na wamekuwa wakitoa fursa ya walimu kujifunza kwa kutoa elimu ya nadharia na vitendo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post