Kundi la wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF) la nchini Sudan limetangaza kuwaachia huru wafungwa 100 wa vita ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Eid el Haji.
Kundi hilo limesema kuwa wafungwa walioachiliwa walinaswa na kutumwa kupigana vita ambavyo havikuwa vyao.
Taarifa iliyowekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Serikali ya Sudan imesema kuwa jeshi linasitisha mapigano katika siku ya kwanza ya Eid al-Adha.
Aidha kulingana na taarifa ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu milioni moja wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano yaliyozuka nchini humo Aprili 4 mwaka huu huku kati ya 3,000 na 5,000 wakipoteza maisha.
Leave a Reply