Wafahamu watu ambao hawana Finger print vidoleni

Wafahamu watu ambao hawana Finger print vidoleni

Inafahamika kuwa kwa sasa suala la usajili kwa kutumia alama ya kidole imekuwa kawaida sana na ili uweze kupata baadhi ya huduma basi inakubidi uweke alama ya kidole (Finger Print) na hii sio Tanzania tu bali hadi katika mataifa mengine.

Inafahamika kuwa kila mtu huwa na alama za vidole ambazo ni tofauti na mwingine hata kama akiwa mzaZi na mwanaye bado alama hizo haziwezi kufanana, watu hutumia alama ya kidole kupata vitambulisho , ‘kadi’ za simu na hata kutumia kama njia ya usalama wa kulinda vifaa vyao kama vile simu.

Lakini jambo hilo limekuwa tofauti kwa familia Apu Sarker iliyopo  Bangladesh ambayo wanafamilia wamezaliwa bila kuwa na alama za vidole jambo linalosababisha wapate tabu kupata baadi ya huduma ikiwemo ‘kadi’ za simu, kitambulisho cha taifa na huduma nyingine.

Inaelezwa kuwa mwaka 2008 katika nchi yao ilianza rasmi mfumo wa kupata kitambulisho cha taifa kwa kutumia alama ya vidole , jambo lililopelekea kuwashangaza waliokuwa wakimuhudumia kwani waligundua hana alama hizo kwenye vidole vyake vya mkono.

Kutokana na tatizo hilo Apu anaeleza kuwa lilimsababishia kukosa baadhi ya huduma muhimu kama vile ‘leseni’ ya udereva, na passport ya kusafiria , baada ya kusumbuka kwa muda mrefu ndipo alifanikiwa kuipata baada ya kupata cheti kutoka kwa madaktari kuwa hana alama za vidole.

Sio yeye tuu mwenye tatizo hilo bali hadi watoto wake kwani wamerithi kutoka kwa mababu zao, jambo hilo linapelekea watoto wategemee alama ya kidole cha mama yao. Kitaalamu tatizo hilo la kukosa alama za kidole hufahamika kama  Adermatoglyphia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post