Kati ya filamu za animation zilizojizolea umaarufu duniani ni Tom na Jerry iliyoanzishwa na mchoraji wa vibonzo William Hanna, raia wa Marekani aliyesomea uandishi wa habari katika Chuo cha Compton Junior huko California na Joseph Barbera, raia wa Marekani aliyesoma katika Taasisi ya Pratt huko Brooklyn.
Wawili hao walikutana katika studio ya MGM iliyopo Hollywood ambapo walifanya kazi kama wachoraji wa vibonzo katika miaka ya 1938 na baada ya miaka miwili Februari 10, 1940 waliamua kutengeneza katuni ya paka na panya iitwayo ‘Puss Gets the Boot’.
Ndiyo ukawa mwanzo wa utengenezwaji wa katuni hizo wakati huo wakitumia majina ya wahusika kama Jasper (paka) na Jinx (panya), kisha baadaye majina ya wahusika katika katuni hiyo yalibadilishwa na kuitwa Tom and Jerry.
Hanna na Barbera walitengeneza katuni 114 wakiwa katika studio za MGM, lakini mambo yalienda kombo baada ya kuongezeka kwa televisheni, filamu zao hazikupewa nafasi sana katika studio hiyo ndipo wakaamua kuanzisha kampuni yao iitwayo ‘Hanna-Barbera Productions’, ambayo ilitengeneza mfululizo wa katuni za televisheni ikiwemo The Flintstones, Yogi Bear, The Jetsons, Scooby-Doo na nyinginezo.
William Hanna alizaliwa July 14, 1910 na alifariki March 22, 2001 akiwa na miaka 90, naye Joseph Barbera alizaliwa March 24, 1911 na kufariki Desemba 18, 2006 akiwa na umri wa miaka 95, licha ya wakongwe hao kufariki lakini ‘Tom and Jerry inaendelea kutamba huku toleo la mwisho likitolewa mwaka 2021 chini ya director Tim Story.
Tom and Jerry ni mfululizo wa katuni za vichekesho za filamu fupi ulioanzishwa mwaka 1940. Unahusu uhasama kati ya wahusika wakuu Tom, paka, na Jerry, panya.
Leave a Reply