Wafahamu Mbwa wasiobweka

Wafahamu Mbwa wasiobweka

Duniani kuna aina nyingi za mbwa, lakini licha ya kuwa na aina hizo wanyama hawa huzoeleka kwa kuwa na mtindo wa kufanana kwenye kubweka.

Mfanano huo wa sauti za kubweka unajionesha kuwa tofauti kwa mbwa aina ya Basenji ambao ndiyo mbwa pekee duniani ambao habweki kabisa.

Licha ya kuwa hawabweki kama mbwa wengine lakini hutoa sauti mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuunguruma, kulia kwa sauti nyembamba na wakati mwingine hutoa sauti kama binadamu akibehua.

Mbwa hawa asili yao ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, dume huwa na urefu hadi sentimita 43 na uzito wa kilo 11, wakati jike huwa na urefu wa sentimita 40 na uzito wa kilo 9.5, kwa kawaida huishi kati ya miaka 14 hadi 16.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post