Vision pro yatumika kufanyia upasuaji

Vision pro yatumika kufanyia upasuaji

Madaktari wa upasuaji kutoka nchini Uingereza, wapatikanao katika Hospitali ya Cromwell jijini London kwa mara ya kwanza wameshika vichwa vya habari nchini humo baada ya kufanikiwa kumfanyia mgonjwa upasuaji wa uti wa mgongo kwa kutumia Apple Vision Pro.

Vision Pro ni kifaa aina ya miwani inayovaliwa na muuguzi ambayo inamsaidia katika hatua zote za upasuaji (operation), kumuelekeza vifaa anavyotakiwa kuvitumia.

Kifaa hicho kilichowekwa program ya AI kutoka katika kampuni ya eXeX iliyopo Marekani husaidia kuongeza ufanisi wa upasuaji kwa kutoa maelekezo pamoja na muongozo wa kimatibabu.

Ikumbukwe kuwa kampuni ya Apple, bidhaa hiyo ilingia sokoni kwa mara ya kwanza Februari 2, mwaka huu, kifaa hicho kinauwezo wa kutumika kama Kompyuta, kutazama movie, kusoma vitabu, kuperuzi mitandaoni nk, ambacho kinaghalimu dola 3,499 ikiwa ni zaidi ya tsh 8 milioni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post