Vijana wajihusishe na kilimo badala ya Ku-bet

Vijana wajihusishe na kilimo badala ya Ku-bet

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeandaa maeneo wezeshi ya kilimo kwa Vijana ili kuwekeza kwenye kilimo na kuwaondoa kwenye maisha ya ku-bet.

Hayo yameelezwa  na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde Jijini Dodoma katika Mkutano na Wahariri uliolenga kutekeleza ushiriki wa Vijana katika kilimo biashara programu inayotarajia kuongeza ajira kwa Vijana 3000 na kuongeza ukuaji wa Sekta ya Kilimo hadi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.

"Vijana wetu wanatamani kufanya kilimo lakini miundombinu ya kuwafanya wakafanya kilimo haikuwa rafiki sana sisi tumeamua kukifanya kilimo kivutie na Vijana watoke kwenye kubet wakalime kwahiyo tulichokiamua tuliweka mazingira rafiki kumfanya Kijana avutike akalime tumeamua kusafisha maeneo na kuweka miundombinu, tutawasaidia miundombinu na tutawatafutia masoko"

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post