Baada ya mwanamuziki kutoka Marekani Celine Dion kuachia ‘trela’ ya filamu yake huku ikiteka vichwa vya habari baada ya kuonekana akimwaga machozi, hatimaye filamu hiyo imeshatoka na kuwahuzunisha wengi baada ya kunesha mateso aliyopita kufuatia na ugonjwa wa ‘Stiff Person Syndrome’ uliomuanza toka mwaka 2008.
Kupitia video hiyo inayosambaa mitandaoni ikimuonesha mwanamama huyo akilia kwa uchungu kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapitia kufuatia na ugonjwa huo uliosababisha kughailisha ziara zake zote.
Filamu ya ‘I Am: Celine Dion’ iliachiliwa rasmi kupitia mtandao wa ‘Amazon Prime Video’ Juni 25, 2024.
Aidha kupitia video hiyo pia ilimuonesha mkali huyo wa ngoma ya ‘My Heart Will Go On’ mwenye umri wa miaka 56 akiendelea kufanya mazoezi ya kuimba licha ya kukutwa na changamoto hiyo.
Ukiachilia mbali msanii huyo kuja na filamu hiyo, Mei 30 mwaka huu chanzo cha karibu cha msanii huyo kiliripoti kuwa #Celine atatumbuiza kwa mara ya mwisho katika kipindi maalumu cha Tv huku ikielezwa kuwa kwa sasa amekuwa akifanya kazi na wakufunzi wa sauti, watu wa bendi na wataalamu kwa zaidi ya miezi sita sasa ili kulikamilisha hilo.
Leave a Reply