Uzinduzi wa The Royal Tour Kitaifa

Uzinduzi wa The Royal Tour Kitaifa

Moja kati ya taarifa kubwa ambayo tumekuletea siku ya leo ni kuhusiana na Kamati ya Kitaifa ya Rais ya Kutangaza Tanzania, imesema kuwa Mei 8, 2022 Filamu ya Tanzania ‘The Royal Tour’ itaoneshwa vituo vyote vya Runinga Nchini ili watanzania wote wapate nafasi ya kuiona.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akitoa taairifa juu ya uzinduzi wa Filamu hiyo utakaofanyika Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Jijini Arusha leo  Aprili 28, 2022.

“Mei 8, 2022 ndiyo itakuwa siku ya kitaifa ya kuzindua Filamu hiyo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC), Dar es Salaam baada ya kuzinduliwa nchini katika kitovu cha utalii Mkoani Arusha Aprili 28, 2022 na Zanzibar Mei 7,2022, tukio hilo litakuwa Mubashara katika Runinga zote nchini”, Dkt. Hassan Abbasi.

Akijinasibu zaidi kuhusiana na Filamu hiyo aliyosema ya kihistoria, Dkt.Abbasi amesema kuwa ni matarajio ya Serikali kuonwa na watu takribani bilioni moja duniani kote katika kipindi cha miezi michache kufuatia tayari kuanza kuoneshwa katika Majukwaa mbalimbali ikiwemo Apple TV inayowafikia watu mil.130 na Amazon Prime milioni 150 duniani kote.

Halkadhalika , Dkt.Abbasi amesema filamu ya Tanzania ya ‘The Royal Tour’imeshaanza kuoneshwa katika Runinga 350 za Majimbo mbalimbali nchini Marekani inayowafikia asilimia 86 ya wamarekani wote zaidi ya mil.200.

Sambamba na hayo Dkt.Abbasi amesema Tanzania ni Nchi ya 9 duniani kushiriki Programu ya Royal Tour ikiwa ni ya pili Barani Afrika na ya Kwanza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post