Uturuki yaongeza mishahara ya wafanyikazi kwa 45%

Uturuki yaongeza mishahara ya wafanyikazi kwa 45%

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametanga kuwa serikali inaongeza mishahara ya wafanyakazi wake kwa asilimia 45, na hii ni siku tano kabla ya uchaguzi mkuu.

Kura za maoni zinaonyesha Erdogan anakabiliwa na kinyang'anyiro kikali kutoka mgombea urais wa upinzani, Kemal Kilicdaroglu.

Uchumi wa Uturuki ni suala muhimu kuelekea uchaguzi wa Jumapili. Kupunguzwa kwa viwango vya riba visivyo vya kawaida vilivyotafutwa na Erdogan kulisababisha kushuka kwa thamani ya lira ya Uturuki mwishoni mwa 2021 na kupelekea mfumuko wa bei kufikia kilele cha miaka 24 cha asilimia 85.5 mwaka jana.

Uchumi unaosuasua wa nchi hiyo, ambao pia unayumba baada ya matetemeko makubwa ya ardhi mwezi Februari, umekuwa pigo kubwa kwa kampeni ya Erdogan ya kuchaguliwa tena.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post