P Square wahamishia ugomvi wao kwenye nyimbo

P Square wahamishia ugomvi wao kwenye nyimbo

Baada ya kutifuana kwa miezi kadhaa katika mitandao ya kijamii wanamuziki kutoka Nigeria ambao pia ni mapasha Peter na Poul Okoye waliounda kundi la Psquare sasa wamehamishia ugomvi wao kwenye nyimbo.

Siku moja iliyopita Peter ‘Mr P’ aliachaia ngoma iitwayo ‘Winning’ kupitia Instagram yake kuwafahamisha mashabiki kwamba ameachia ngoma mpya, lakini suala hilo lilizua taharuki baada ya kaka yake Poul ‘Rudeboy’ kusema kuwa wimbo huo ni wake.

Aidha baada ya Mr P kushare kionjo kidogo cha wimbo huo naye pacha wake Rudeboy alishare kionjo kinachoendana na wimbo huo huo huku akidai kuwa huo ni wimbo wake na alipanga kuuachia mwakani kwenye album yake.

“Title ya wimbo: WINNING, Imeandikwa na kuimbwa na RUDEBOY, Imetayarishwa na mtayarishaji huyo huyo. Sasa imekuwaje? Je, inabidi nitoe toleo lingine? Bwana Mtayarishaji”,

“Wewe ni kesi ya siku nyingine kabisa, ni jambo rahisi tu uliambiwa ulete nyimbo 6 nami nilete nyimbo 6, nikawasilisha katika uongozi sasa kwanini unaimba tena wimbo wangu mwenyewe neno kwa neno, Wimbo ambao ulikuwa uwe kwenye albamu yangu Juni mwaka ujao” ameandika Rudeboy

Ikumbukwe kuwa mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu Paul Nonso Okoye ‘Rudeboy’ alithibitisha kusambaratika kwa kundi la PSquare kwa mara nyingine kwa kudai kuwa toka walivyoungana hakuna cha maana kilichowahi kufanyika.

Kundi la P-Square lilisambaratika kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na kuungana tena mwaka 2021, huku mwishoni mwa mwaka jana walikiwasha tena ambapo mpaka kufikia sasa bado hawajapatana.

Wawili hao walitamba na ngoma zao kama ‘Taste The Money (Testimony )’, ‘Personally’, ‘Forever’ pia wamewahi kutoa kolabo na mwanamuziki Diamond wimbo uitwao ‘Kidogo’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags