Utafiti: Kumbusu mpenzi wako asubuhi kutakusaidia kuishi maisha marefu

Utafiti: Kumbusu mpenzi wako asubuhi kutakusaidia kuishi maisha marefu

Mtindo wa maisha wenye afya, kula mlo wenye virutubishi kamili, kuishi katika mazingira salama na yenye kuridhisha, kufanya mazoezi, na kuishi maisha yasiyo na wasiwasi, msongo, na hofu ni baadhi ya mambo yatakayofanya uishi maisha marefu.

Lakini mbali na haya, jambo jingine ambalo linaweza kumfanya mtu aishi kwa muda mrefu ni kumbusu.

Kulingana na mtaalamu wa saikolojia kutoka Ujerumani, Dr. Arthur Sazbo ameeleza kuwa kumbusu mwenzi wako asubuhi kunaweza kukusaidia kuishi maisha marefu na kuanza siku yako kwa mtazamo mzuri.

Mbali na hayo pia ameweka wazi kuwa kumbusu mpenzi wako kuna faida nyingine nyingi za kiafya zikiwemo kuimarisha Afya ya Akili, kusaidia asipate na matatizo ya Ugonjwa wa moyo (hii mara nyingi inapunguza shinikizo la moyo), kunaimarisha afya ya meno, kinga pamoja na kujenga uhusiano mzuri na wa muda mrefu.

Aidha alieleza kuwa kulingana na utafiti wake watu wanao wabusu wapenzi wao kila siku asubuhi wanauwezekano wa kuishi kuanzia miaka mitano na kuendelea kuliko wale ambao hawafanyi hivyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags